MKAZI wa Igunga, Kada wa CCM, Mussa Tesha
aliyekuwa katika matibabu India baada ya kumwagiwa tindikali usoni na
watu wanaodaiwa kuwa wa CHADAEMA, wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo
jimboni humo mwaka jana, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es
Salaam, baada ya kurejea nchini. Kulia ni Katibu wa NEC, Uchumi na
Fedha Mwigulu Nchemba ambaye alikuwa Meneja wa Kampeni za CCM jimboni
humo.
Na Mwandishi Wetu
KADA wa CCM, mkazi
wa Igunga, Tabora, Mussa Tesha (24) aliyekuwa akipatiwa matibabu
India, baada ya kuwagia tindikali na watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa
Chadema wakati wa kampeni za uchagfuzi mdogo jimboni humo mwaka jana,
amerejea nchini.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Uchumi
na Fedha Mwigulu Nchemba alisema leo kwamba, Tesha amerejea juzi,
akiwa amepona kiasi cha kuweza kuzungumza na kuona jicho moja huku
lingine likiwa bado halioni vizuri kutokana na athari alkizopata
Akizungumza
nyumbani kwake Tegeta Mwisho, Dar es Salaam, Mwigulu ambaye alikuwa
Meneja wa Kampeni za CCM Igunga, alisema amemhifadhi Tesha nyumbani
kwake wakati akisubiri kwenda tena India kuendelea kuendelea na
matibabu madogo yaliyosalia.
Mwigulu alisema, Chama Cha Mapinduzi ambacho
kiligharamia matibabu yote, hadi sasa kinaendelea kumhudumia Tesha mpaka
atakapopona kabisa na kuwa na uwezo wa kufanya kazi.
"Hadi sasa
tunashukuru kwamba amepona anaweza kuzungumza, kusikia na kuona walau
jicho moja, tofauti na mwanzo alivyokuwa mara alipomwagiwa tindikali,
hata hivyo hali yake haijaweza kuwa ya kufanya kazi mbalimbali kama za
juani, hivyo CCM tunaendelea kumsaidia mpaka ajenge uwezo wa
kujitegemea", alisema.
Alisema, CCM imefanya mpango wa kuwaugnanisha
wabunge wa CCM kumtayarishia mtaji ambao utamsaidia Tesha kuendesha
maisha yake baada ya kukumbwa na madhara hayo.
Akizungumza kwa
mara ya kwanza tangu amwagiwe tindikali, Tesha amewashukuru Watanzania
kwa kumuombea wakati wote alipokuwa mgonjwa na kwamba anaamini dua zao
ndizo zimemwezesha kubakia hai hadi sasa.
Tesha alisema,
baada ya kumwagiwa tindikali Septemba 9, mwaka jana, hakujitambua hadi
alipokuwa katika hospitali ya KCMC ambako alipatiwa matibabu na baadaye
kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alikaa wiki tatu kabla
ya kupelekwa India.
No comments:
Post a Comment