LICHA ya Waziri Mkuu, Mizengo
Pinda kutoa amri kwa madaktari wote wenye mikataba na Serikali kurejea
kazini, bado wanataaluma hao jana waliendeleza mgomo baada ya kutia
saini vitabu vya mahudhurio na kutoweka kusikojulikana huku wauguzi
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), wakitoa msimamo mpya kwamba
hawako tayari kufanya kazi na madaktari kutoka Jeshi la Ulinzi la
Wananchi (JWTZ).
Juzi, Waziri Mkuu Pinda alitoa
onyo kwa madaktari hao akiwataka kurejea kazini kufikia jana kinyume
chake ambaye angeshindwa angekuwa amejifukuzisha kazi na kwamba
madaktari wa JWTZ wangechukua nafasi zao.
Agizo hilo la kwamba
wangewatumia madaktari kutoka JWTZ jana liliamsha hasira za wauguzi
Muhimbili ambao walitangaza msimamo wao wa kutofanya kazi nao.
Mwenyekiti wa Chama cha Wauguzi
Tanzania, Tawi la MHN, Paul Magesa alisema madaktari hao hawana uwezo
wa kufanya kazi katika hospitali hiyo ya taifa ambayo ndiyo kubwa nchini
kwa kuwa inahudumia wagonjwa walioshindikana katika hospitali
wanazotoka.
“Sisi tulishafanya kazi nao
mwaka 2005 na tunawafahamu wengi hawajui mambo mengi, watakuja kutuuliza
na kutuongezea kazi za kufanya… tunaomba katika hili Serikali isikwepe
tatizo, ilishughulikie kwa maslahi ya taifa,” alisema Magesa.
habari imeandikwa na gazeti mwananchi.
No comments:
Post a Comment