Mchezaji
Mwanahamisi Omari a.k.a Gaucho akihojiwa na mwandishi wa habari wa BBC
Eric David Nampesya baada ya kumalizika kwa mpira kati ya Twiga Stars na
Namibia , Mwanahamis
Omari 'Gaucho' ni mfungaji pekee wa mabao 2 kati ya 5 ya Twiga,
katika mchezo wa kutafuta kufuzu kwa fainali za Afrika kwa Wanawake,
zinazotarajia kufanyika mwezi Juni mwaka huu.
Mchezo huo umemalizika muda mchache katika uwanja wa Taifa.
Mabao
ya Twiga yalifungwa na Mwnahamisi Omar katika dakika 21, Asha Rashid
'Mwalala', bao la pili dakika 46, bao la tatu Etoe Mlenzi, dakika ya
84, Asha Rashid,bao la nne dakika ya 88, na bao la tano, likifungwa tena
na Mwanahamis, dakika ya 90. Mabao ya Namibia mawili ya yamefungwa na
Beki wa Twiga, Etoe, aliyejifunga dakika ya 29 na bao la pili
likifungwa na Juliana Skrywer, dakika 73.
Kwa
matokeo hayo sasa Twiga Stars inatarajia kukutana na mshindi kati ya
Misri au Ethiopia ambapo Misri ilikuwa inaongoza kwa mabao 4-2 dhidi ya
Ethiopia.
Mchezaji
wa timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania Twiga Stars Asha Rashid
akimtoka beki wa timu ya taifa ya Namibia ya wanawakeLovisa Mulunga,
katika mchezo wa kuwania fainali za kombe la dunia kwa wanawake
unaochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jioni hii,
No comments:
Post a Comment