Wachezaji wawili wanaoweka ngumu kusaini mkataba mpya ndani ya klabu ya Manchester United Paul Pogba na Ezekiel Fryers wameambiwa wasaini mikataba mipya ndani ya masaa 48 au wasahau kuichezea tena Manchester United.
Teenagers
hao wanaonekana kutaka kufuata mfano wa bad-boy Ravel Morrison nje ya
Old Trafford baada ya kukataa kuweka saini kwenye mikataba mipya kwa
muda mrefu sasa.
Pogba
18, na Fryers 19, wanamaliza mikataba yao mwezi June mwaka huu na baada
ya kubembelezwa sana sasa inaonekana mabosi wa United wamepoteza
uvumilivu na kuawaambia ijumaa ndio mwisho na hatma yao wataichagua siku
hiyo.
No comments:
Post a Comment