Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, April 27, 2012

BABA MZAZI WA KANUMBA AONGELEA ISSUE YA MAMA KANUMBA KUVURUGA MIRATHI...!!!





Marehemu Steven Kanumba na Baba yake Charles Kaumba
---
Baba mzazi wa Kanumba anaeishi Shinyanga amefunguka na , kuzungumza Exclusive na millardayo.com na kusema kwamba sasa yuko tayari kuja Dar es salaam kushughulikia swala la Mirathi baada ya kudai kwamba mama mzazi wa Kanumba ambae yuko Dar ameanza kuharibu issue ya mirathi.
Amesema “Tutakaa kikao Jumamosi kuteua msimamizi wa mirathi, mama ameteua kinyemela bila kunishirikisha, hilo swala nimelipinga nimewasiliana nae kumuuliza kwa nini kafanya hivyo akawa ana jiuma uma tu, kwa nini umeokota watoto kuwadanganya danganya kikao cha kusimamia mirathi si tungekaa pamoja? akachukua watoto wangu wako huko wasichana wawili lakini walipotoka kikaoni wakanipigia simu kwa sababu hawakuridhika.”
Baba huyu mzazi wa Kanumba amezidi kufunguka kwamba “mama hakusema lolote baada ya mimi kumwambia huo mkutano ni batili lakini akauliza kwani yeye akiteuliwa peke yake kuna ubaya gani, nikamwambia ingekua halali kuteuliwa peke yako kama tungekua tunaishi pamoja lakini tulishatengana kwa hiyo pande zote mbili ni lazima ziteue, huyu mama aliwateua hao watoto wangu wawili alafu akamchukua kinyemela na kumlipia nauli kijana wangu mwingine anaitwa Ayubu ambae ni mtoto wa dada yangu.”
“Tulikubaliana kwamba mpaka tufanye siku 40 za marehemu sasa yeye kaanza kukaa kinyemela tena, maajabu maajabu.. sasa hivi tunakaa huku huku kikao cha wa wanandugu cha mzee Kanumba wanatoka Sengerema Mwanza na Bariadi Shinyanga, kama wakiniteua kwenda Dar es salaam nitakwenda.”

No comments:

Post a Comment