Aliyekua
mlinzi wa zamu kwenye jengo la Amani lililoko mtaa wa Ohio Dar es
salaam, jengo ambalo ilifanyika video ya NAI NAI ya Ommy Dimpoz na Ally
Kiba, Mganga Msabila aliyekua ameajiriwa na Ultimate Security ameamua
kuacha kazi hiyo ya ulinzi baada ya video hiyo kumletea matatizo kazini.
Mganga
amesema “tumepata mamtatizo wakati meneja mwenyewe wa jengo aliruhusu
hiyo video ifanyike japo alionya kwamba tuhakikishe kina Ommy Dimpoz
hawachafui eneo wala kuharibu chochote, siku ya tukio walifanya video
yao na mpaka tunakabidhi lindo walikua wanaendelea”
Kwenye
sentensi nyingine, Mganga amesema “baada ya siku mbili tuliitwa kwenye
makao makuu ya kampuni yetu kule Ultimate Security tukaenda kuandikisha
maelezo jinsi ilivyokua, baada ya pale tulijua ishu imekwisha na mwaka
2011 ukamalizika manake video ilifanyika november, lakini tukashangaa
tukaja kuitwa tena February 2012 tukaitwa tena makao makuu kutoa maelezo
sisi tumeruhusuje ile video kufanyika pale, ishu iliibuka upya baada ya
wenye jengo kuona ile video inapigwa sana kwenye TV na pia wanasema ina
Ommy Dimpoz wamecheza mpaka ndani ya jengo lakini mimi mpaka nakabidhi
lindo kina Ommy Dimpoz hawakua wameingia ndani”
Msabila
ambae ni baba wa watoto wanne ambao wanamtegemea peke yake huku mkewe
akiwa ni mama wa nyumbani, ameamplfy zaidi kwamba “wenye jengo
walikasirika baada ya kuona hiyo video wakatuma tena Taarifa kula makao
makuu ya kampuni yetu na walituma na cd nzima ya ile video na wakawa
wanahoji kwa nini hawa walinzi waliokuepo zamu siku hiyo hawajafanyiwa
kazi? kitu ambacho kilitupa adhabu ya kukatwa mshahara kwa muda wa miezi
sita au mwaka kwa sababu wanasema wanatuchunguza, kwa hiyo nikaona
haina haja ya kuendelea na kampuni yao ngoja niondoke tu, kosa sio langu
limekuja kuwa langu lakini sisi ndio tunashushiwa hayo mambo, nimeona
nisije nikaangamiza wengi kwa kosa hilo dogo ngoja nijiengue na
mwenzangu nae amejiengua”
Mganga
Msabila ambae alipita jeshini kabla ya kuanza kufanya kazi ya ulinzi
chini ya kampuni binafsi, kwa sasa amerudi kijijini kwao Sengerema
wilayani Chanika mkoani Mwanza ambako ndio familia yake ilipo, anasubiri
kama itatokea tena akapata nafasi ya kazi ya ulinzi popote, Ommy Dimpoz
ameahidi kuzungumza na millardayo.com
No comments:
Post a Comment