Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee la YANGA, Mzee Ibrahimu Akilimali (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari.
BARAZA la Wazee la klabu ya Yanga ya Dar es Salaam imeamua
kuichukua timu ili kuiandaa na mechi dhidi ya wapinzani wao wa jadi, Simba SC
Mei 5, mwaka huu kufuatia mgogoro unaoendelea klabuni.
Asubuhi ya leo, wazee wa Yanga wakiongozwa na Katibu wao Mkuu,
Ibrahim Ally Akilimali walifika makuu ya klabu, makutano ya mita ya Twiga na
Jangwani, Dar es Salaam na kufanya Mkutano
na Waandishi wa Habari.
Katika Mkutano huo, Mzee Akilimali alisema maamuzi hayo yana
Baraka za Mwenyekiti wa klabu, Wakili Lloyd Baharagu Nchunga.
Kwa sasa Yanga ipo katika mgogoro, kufuatia Wajumbe wake
wawili wa Kamati ya Mashindano na Usajili, Abdallah Ahmed Bin Kleb kujiuzulu
kwa kutoridhishwa na mwenendo wa uongozi.
Machi mwaka jana, aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Yanga,
Davis Mosha naye alijiuzulu kwa sababu za kutoelewana na Mwenyekiti wake,
Nchunga.
Yanga iliyopoteza matumaini hata ya kushika nafasi ya pili kwenye
Ligi Kuu, inaingia kwenye mechi dhidi ya watani wa wa jadi, Simba walio katika
hali nzuri.
Kwanza wana uhakika wa kuchukua ubingwa na pili
wanaendelea vizuri kwenye michuano ya Afrika, kesho wakicheza mechi ya kwanza
ya hatua ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Ahly Shandy ya
Sudan.
No comments:
Post a Comment