Roma
Mkatoliki akitumbuiza jukwaani wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Tanzania Music
Award jijini Mbeya katika Uwanja wa Sokoine jana. Kwa hisani ya http://mrokim.blogspot.com
Suma
Lee nae alishambulia jukwaa vilivyo na kuleta raha kwa mashabiki katika wakati
wa show maalum ya Washindi wa Kili Tanzania Music jijini Mbeya
Ben
Paul nae alishambulia jukwaa vilivyo na kuleta raha kwa mashabiki katika
wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Tanzania Music Award jijini Mbeya.
Barnaba
Boy ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Mwimbaji Bora wa Kiume akimba jukwaani
jana wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Tanzania Music Award
jijini Mbeya katika
Uwanja wa Sokoine
Vijana wengi walikuwa wamepigilia vitu vya namna hii
Mashabiki walikuwa hawatulii
Mkali
wa Bongo fleva Ali Kiba akiimba jukwaani
hii wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Tanzania Music Award iliyofanyika uwanja
wa Sokoine
Wasichana waliokuwa wakitoa huduma ya tiketi
Mkali
wa Bongo fleva Ali Kiba akiimba na Omy Dimpoz katika wimbo Nai Nai jukwaani
hii wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Tanzania Music Award iliyofanyika uwanja
wa Sokoine
Dimpoz kwa Pozi akipitika katikati ya wacheza show wake.
Msanii
AT kutoka Zanzibar akitumbuiza jukwaani na wacheza show wake wakati wa show
maalum ya Washindi wa Kili Tanzania Music Award jijini
Mbeya katika Uwanja wa Sokoine jana
Back Stage mambo yalikuwa hivi, Toka kushoto ni Ali Kiba, Omy Dimpoz, Ben Pol na Meneja wa Omy Dimpoz Mubenga. Kwa hisani ya http://mrokim.blogspot.com
***********************
MANENO ya Injili yanayosema Wamwisho
anakuwa wakwanza na wakwanza akawa wamwisho yametima jana katika Uwanja wa
Sokoine Mjini Mbeya pale mkali wa Hip Hop,
Roma Mkatoliki alipoongoza jahazi
la wakali wa Tuzo za Kili Tanzania Musc Awards 2012 katika onesho lao la Uwanja wa
Sokoine mjini Mbeya jana.
Roma akipanda jukwaani
akisindikizwa na DJ maarufu DJ Choka, alishangiliwa vilivyo na umati wa watu
uliofurika uwanjani hapo pale tu ilipofika zamu yake kupanda.
Roma! Roma! Roma! Roma!....hayo ndio
yalikuwa maneno ya shangwe kutoka kwa wapenzi wa burudani kutoka Jijini Mbeya
waliofurika katika Uwanja wa Sokonine mjini hapa kushuhudia show hiyo kali ya
Washindi wa Tuzo za Kili Tanzania Music Awards 2012.
Roma baada ya kumaliza kuimba nyimbo
zake kwanza aliwashukuru wana Mbeya kwa kura zao zilizompa ushindi na kuwaambia
sasa anamaliza show hiyo ambayo hadi hapo alipofikia alisema wametumia Sh 200/=
pekee kati ya Sh 2,000 ya kiingilio waliyotoa.
“Sasa ndugu zangu, nawaambia ukweli hadi
sasa mmeshatumia sh 200 tu ya kiingilio chenu,..sasa nawapa show ya Sh 1,800
iliyobaki,” alijigamba Roma ambaye muda wote alikuwa akishangilia na ndipo
alipomaliza kwa kuimba Wimbo wa Mathematics uliompa tuzo.
Wasanii wengine waliopanda jukwaani
jana ni pamoja na Ben Pol, AT, Ali Kiba , Barnaba, Omy Dimpoz na Suma Lee nao wamefunika vibaya katika
Tamasha la Kili Music Award Winners Tour lililofanyika katika Uwanja wa sokoine
Mjini Mbeya.
Alianza jukwaani kupanda mshindi wa Tuzo ya wimbo Bora wa R&B,Msanii
Ben Paul ambaye alijinyakulia tuzo hiyo kupitia kibao Number One ambapo nae
alishambulia jukwaa na kuwaamsha watu kuwa sasa show imeanza.
Alifuata jukwaani Suma Lee ambaye
aliongozwa na show kali kutoka kwa vijana wake wanne wakike na wakiume na
kushangiliwa vilivyo kwa mkongwe huyo wa Bongo Fleva.
Baada ya Ben Pol, alipanda mkali kutoka
Zanzibar ambaye ni mshindi wa Tuzo Wimbo Bora wenye Vionjo vya Kiasili AT na
kutoa burudani ya nguvu na wimbo wa Vifuu Utundu ambao ulimpa tuzo aliucheza
vilivyo na wanenguaji wake wawili wa kike.
Ikafika zamu ya Omy Dimpoz jukwaani kwa
kuimba nyimbo yake mpya ambayo alitaraji kuizindua jana katika Ukumbi wa Club
Bilicanas jijini Dar es Salaam, single ya Baadae kisha ikafuata ile iliyompa tuzo ya Wimbo bora wa
Kushirikiana Nai Nai aliyoanza kuimba peke yake na baadae kuurudia wimbo huo
akiwa na Ali Kiba.
Ali Kiba alibaki jukwaani hapo kama
ilivyokuwa mjini Moshi na vijana wake kumfuata kutoa shukrani zao za kupata
kura zilizowapa ushindi wa tuzo ya Wimbo bora wa Zouk Rhumba kupitia wimbo wa
Dushelele.
Wakati mara zote pazia la utoaji
burudani kwa washindi hao wa tuzo za Kili Music Award 2012 wanaofanya ziara limekuwa
likifunga na Roma Mkatoliki akapanda wa pili kutoka mwisho.
Roma
ambaye ni Mshindi wa tuzo mbili za Wimbo Bora wa Hip Hop kupitia wimbo wake wa
Mathematics na Tuzo ya Msanii bora wa Hip Hop, alishambulia jukwaa huku
viitikio vyake vikiimbwa na DJ Choka na hata alipomaliza show yake bado
mashabiki walimtaka aendelee.
Mshindi wa Tuzo ya Mwimbaji bora wa
Kiume, Barnaba ndiye aliyefunga pazia hilo mjini Mbeya kwa
kuimba ikiwapo inayovuma kwa sasa ya
Magube Gube.
Wasanii
hao wiki ijayo wanataraji kutoa burudani kama hiyo jijini Mjini Mtwara na
tayari walisha tumbuiza na kuwashukuru mashabiki wao wa Mkoani Dodoma na Jijini
Mwanza na Moshi.
Kwa hisani ya http://mrokim.blogspot.com
No comments:
Post a Comment