Taarifa
zilizothibitishwa kutoka ndani ya klabu ya Simba zinasema uongozi wa
timu hiyo umewatupia vilago nje wachezaji wake Derrick Walulya kutoka
nchini Uganda na Gervas Kago kutoka Jamhuri ya Kati ambao waliitumikia
klabu hiyo msimu wa ligi uliomalizika.
Hatua
hiyo pengine imekuja baada ya wachezaji hao kuchezea benchi karibu
msimu mzima wa ligi wakiwa nje ya uwanja ukiacha Gervas Kago ambaye
angalau kwa michezo kadhaa ya Ligi kuu ya Vodacom alikuwa akiingia
dakika chache kabla ya kuisha kwa mchezo.
Hii inaonyesha kuwa Simba watasajili wachezaji wengine ili kuziba mapengo ya wachezaji hao ambao wamewaacha.
No comments:
Post a Comment