Mbunge wa Jimbo la Ubungo Mh.John Mnyika alipokuwa akiwasili Mahakamani leo asubuhi.
Mbunge
wa Jimbo la Ubungo kwa Tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA),Mh. John Mnyika akiwa amebebwa juu juu na Wanachana wa Chama
hicho pamoja na washabiki wake nje ya Mahakama Kuu kanda ya Dar es
Salaam leo mara baada ya kushinda kesi yake iliyokuwa ikimkabili
kuhusiana na Ushindi wake kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010
Wanachama
wa Chadema pamoja na washabiki wa Mbunge wa Jimbo la Ubungo
wakishangilia ushindi wa kesi ya Mbunge wao,Mh. John Mnyika
Mnyika akipongezwa na Baadhi ya jamaa zake waliofika Mahakamani hapo.
Askari
Polisi wakihakikisha usalama upo wa kutosha katika njia walizokuwa
wakipita wapenzi wa Chadema kusherehekea ushindi wa Mbunge wao.Mh. Mnyika alipokuwa akiwasili Mahakamani leo asubuhi.
Wafuasi
na Wanachama Wa Chama Cha demokrasi na Maendeleo CHADEMA wakiwa kwenye
maandamano katika barabara ya bibi titi mohamed kuelekea ubungo mara
baada ya Mbunge wa Jimbo la Ubungo Mh John Mnyika Kuibuka Kidedea katika
Kesi ya Ubunge wa Jimbo la Ubungo iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea
wa Ubunge Jimbo hapo Bi Hawa Ng'umbi katika Uchaguzi Mkuu Uliofanyika
Mwaka 2010
No comments:
Post a Comment