Mashabiki wa shindano la Big
Brother Afrika, leo tena wamepata pigo jingine baada ya Washiriki wa
Nigeria, Ola na Chris kuomba kujitoa kwenye shindano hilo ambapo hiyo
imetokana na Ola ambae anadaiwa kuwa mgonjwa wa bp kuwa dawa alizopewa
hazijafanya kazi hivyo ni lazima atoke kwenye jumba la big brother ili
kuwa karibu zaidi na matibabu ya uhakika.
Chris ambae ni mshiriki
mwenzake walietoka pamoja kwenye jumba hilo, amehuzunika sana kwa
kilichotokea kwa mwenzake na kukiri kwamba anaelewa, walikua kwenye
mashindano wakicheza pamoja lakini hawawezi kucheza na maisha yao.
Baada ya ombi hilo Big Bro
aliwakubalia kuondoka, na ikabidi wawaage washiriki wenzao leo leo na
kuondoka japo wenzao waliwaruhuru kuondoka kutokana na hali halisi,
huzuni ilitawala, washiriki wengine waliobaki walihuzunika sana na
wengine hata kulia kabisa kwa sababu bado walipenda kuendelea kukaa na
Chris na Ola.
Washiriki hao wawili
wanakamilisha idadi ya washiriki watano walioondoka ndani ya jumba hilo
kwa mwaka huu wakiwemoa watanzania wawili pamoja na mzimbabwe mmoja japo
Chris na Ola wametoka bila utaratibu wa kawaida wa washiriki kutolewa
kwenye jumba hilo ambapo huwa ni kila jumapili.
MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2024
-
Bofya Hapa kutazama matokeo
MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2024
26 minutes ago
No comments:
Post a Comment