Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, May 21, 2012

WAKAZI WAWILI IRINGA WAVAMIWA WAPIGWA RISASI


Isa Chatira toka Pawaga mfanyabiashara ya Mafuta aliyevamiwa na kupigwa Risasi akiwa hospitali ya Mkoa wa Iringa.
Gerald Sanga akiwa hopitali baada ya kureruhiwa kwa risasi

WAKAZI WAWILI WAVAMIWA KWA RISASI IRINGA

Watu wawili kutoka katika sehemu tofauti na kwa nyakati tofauti katika Mkoa wa Iringa wamevamiwa na kupigwa na risasi watu wasiojulikana.
Akiongea mmoja wa majeruhi hao aliyetambulika kwa jina la Gerald Sanga toka Ifunda ameeleza kuwa usiku majira ya saa nane akiwa nyumbani alisikia sauti ya mbwa akibweka na kujaribu kutoka nje ili kuangalia ndipo alipopigwa na kudondoka chini huku watu hao waliotenda tukio hilo kutokomea pasipo julikana.
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo aliyejulikana kama ibrahimu anaeleza kuwa majeruhi huyo anaishi na bibi yake ambaye ni mfugaji wa ng’ombe na kwa mujibu wa maelezo yake anasema kuwa uvamizi huo ulikuwa na lengo la kuchukua fedha ambazo zimepatikana kutokana na uuzaji wa mifugo hiyo lakini bila mafanikio walikimbia na kumjeruhi kijana huyo.
Katika tukio jingine eneo la kinyika Pawaga katika mkoa wa IRINGA kijana aliyetambulika kwa jina Isa Chatira(32) mfanyabiashara anayejishughulisha na uuzaji wa mafuta alivamiwa na watu wasiojulikana waliokuja kwa lengo la kununua mafuta.
Akizungumza huku akiwa na maumivu makali Chatira amesema alikuwa kwake baada ya kufunga biashara lakini walitokea wateja ambao walimtaka awauzie mafuta Lakini kabla ya kuwahudumia walimpiga risasi eneo la tumboni na kutokomea pasipo julikana.
Kwa mujibu wa maelezo ya baba wa Isa, Athumani Chatira anaeleza kuwa mwanae huyo ambaye ni mfanya biashara wa mafuta aina ya petrol alivamiwa na watu wasiojulikana. Athumani amezidi kubainisha kuwa kwa mujibu wa Xray iliyofanyika katika hospitali ya mkoa wa Iringa inaonesha kuwa hakuna risasi iliyoingia lakini bado majeruhi yupo katika hali mbaya.
Bado mtandao unazidi kufuatilia habari hizi toka kwa maafisa usalama na madaktari ili kupata ukweli……..

No comments:

Post a Comment