NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE-ARUSHA
WANANCHI wenye hasira katika eneo la Ngusero Ndani ya
manispaa ya Arusha wamewaua majambazi matatu kwa silaha za jadi mara baada ya
majambazi hayo kubainika kuwa wanapanga mbinu mbalimbali za kuvunja nyumba
Akiongea na waandishi wa habari mapema leo kamanda wa polisi
wa mkoa wa Arusha Bw Thobias Andengenye alisema kuwa tukio hilo
lilitokea alfajiri ya saa kumi za asubui ambapo majambazi hayo yalifika katika
eneo hilo huku
yakiwa ndani ya gari
Kamanda Andengenye alisema kuwa mara baaada ya majambazi
hayo kufika katika eneo hilo la tukio wakiwa na
gari aina ya Corola lenye namba T830 AHU walianza kuzunguka zunguka katika eneo
hilo ili
kupanga nyumba ambayo wanaingia hali ambayo iliwashitua wananchi
Alifafanua kuwa mara baada ya wananchi kutilia shaka gari hilo
ambalo lilikuwa na majambazi hao waliamua kuwaweka chini ya ulinzi na kukagua
gari hilo ambapo walikutana na Silaha za jadi
pamoja na silaha nyingine ambazo ni za kuvunjia nyumba hali ambayo ilisababisha waweze
kupigwa sana na wananchi hao
“inavyosemekana ni kwamba hawa majambazi walikuwa
wameshazunguka san a na gari lao kwa muda mrefu sana na sasa mara baada ya
kuhisiwa wananachi waliamua kujichukulia sheria mkononi na kisha kuanza
kuwapiga sana hali ambayo ilisababisha Mauti yao hapo hapo”alisema kamanda
Andengenye.
Aliongeza kuwa mara baada ya Jeshi la Polisi kufika katika
eneo hilo waliweza kugundua kuwa kati ya
majambazi hayo matatu mawili yalikuwa yanatafutwa na jeshi hilo bila mafanikio kwa kuwa walikuwa
wanatuhumiwa kwa makosa ya unyanganyi wa kutumia silaha ndani ya maeneo
mbalimbali ya Mji wa Arusha
No comments:
Post a Comment