Usiku wa May 29 kuamkia may 30 2012 saa nane na dakika kumi ndani ya Maisha Club Dar es salaam, Wema alivishwa pete na mwimbaji Mwinyi wa Machozi Band ambae kwenye hiyo movie yeye atazicheza nafasi zote za Mwimbaji Diamond Platnums aliyewahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Wema Sepetu, Mwinyi amecheza kama Diamond ambae pia alimvisha Wema pete ya uchumba hapohapo Maisha Club.

Mwinyi
alisema huyu ndio mwanamke nilietulia nae baada ya kuzunguka huko kote
na nahitaji awe wangu wa maisha, ni maneno ambayo Diamond aliyasema siku
ya kumvisha Wema Pete.
Mrembo huyu ambae ni Miss Tanzania 2006 amesema mwanzoni alikua anataka hii movie wacheze Irene Uwoya na Jb na ilikua haikua ikihusu maisha ya Wema lakini baada ya Jb kuwa na kazi nyingi, alifikiria kucheza movie mwenyewe na kupewa idea ya Super Star na msanii Suma Lee.
Alichofanya baada ya kupewa hiyo idea na Suma Lee ni kuipimp na kuongeza matukio mengi aliyokutana nayo kwenye umaarufu na ni movie ambayo mastaa wengi wa kibongo wameuza sura ndani yake.

Yote
hii ilikua inarekodiwa na ni sehemu ya hiyo movie mpya ya Wema, sio
kweli kwamba Wema na Mwinyi ni wachumba, hapa ni sanaa tu.








No comments:
Post a Comment