Hatimaye
klabu ya Orlando Pirates imetuma rasmi barua ya mualiko kwa mchezaji wa
Simba Emmanuel Okwi kwenda nchini South Africa kwa ajili ya kufanya
majaribio ya kuweza kujiunga na timu hiyo.
![]() |
Hii ni sehemu ya barua ya Orlando kumualika Okwi. |
Nimefanikiwa
kuiona barua hiyo ikiwa inatoa maelekezo kwamba Okwi atapewa majaribio
ya wiki mbili na Orlando Pirates, huku akihudumiwa kuanzia usafiri,
malazi, matibabu pamoja na gharama nyingine zitakazojitokeza kwa wakati
atakaokuwa na klabu hiyo.
Kwa
kipindi cha misimu miwili sasa Orlando wamekuwa wakimfuatilia Okwi
ambaye klabu yake ya Simba imemuwekea price tag ya Billioni 2 kwa timu
inayomtaka, huku pia wapinzani wao wa jadi klabu ya Yanga ikiwa
inamfukuzia mshambuliaji huyo wa Uganda ambaye siku za hivi karibuni
amekuwa ndio tegemeo la safu ya ushambuliaji ya mabingwa wa Tanzania.
SOURCE SHAFFIH DAUDA
No comments:
Post a Comment