Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, June 10, 2012

Muasisi wa Chama cha Chadema bob makani Afariki Dunia






                                
Kwa taarifa zilizopatikana  muda mchache uliopita zinaeleza kuwa aliyekuwa Muasisi wa CHADEMA, Mohammed "Bob" Makani amefariki Dunia jana jioni  jijini Dar kwenye hospital ya Aghakhan,Mwenyekiti wa CHADEMA amethibitisha hilo kwa njia ya simu kutoka Kanda ya kusini walikokuwa wakifanya mikutano yao ya hadhara.

Mh Mbowe amesema kuwa Marehemu Makani alikuwa akiugua kwa muda mrefu na kupelekwa hospitali mbalimbali kwa matibabu ikiwemo nje ya nchi,amesema kuwa Mwili wa Marehemu umehamishiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa hifadhi.  Msiba upo nyumbani kwake Mbezi Beach jirani na Rainbow.

No comments:

Post a Comment