
Shedrack Nsajigwa mwenye jezi ya kijani.
Nahodha wa Taifa Stars Shedrack
Nsajigwa ambae alikua akiichezea club ya Yanga amesema haitatokea hata
siku moja akaomba mkataba mpya Yanga kwa sababu anajiamini yeye ni
mchezaji mzuri.
Amesema “mimi mkataba wangu na
Yanga umeshaisha kwa hiyo mimi ni mchezaji huru, nilijua siwezi kuwepo
Yanga milele… mkataba umeisha naangalia mambo mengine kwa sababu
nilisaini mkataba wa miaka miwili nikijua siku moja nitaondoka”
Kuhusu yeye kuomba mkataba
mwingine baada ya aliokua nao kumalizika, Nsajigwa amesema “mimi ni
mchezaji bwana najiamini na kazi yangu, siwezi kuomba mkataba bado nguvu
ya kufanya kazi ninayo siwezi eti kuomba mkataba na timu fulani, aaah
never…. sijawahi na haitatokea”
Inaaminika kwamba Nsajigwa
ametemwa Yanga kwa sababu alikua kiongozi wa wachezaji wenzake kugoma
kwa kudai malipo yao, stori nyingine ambazo hazijathibitishwa ni kwamba
Club hiyo inampango wa kuwaondoa wachezaji wote wenye umri mkubwa na
kutaka damu changa kwa ajili ya msimu ujao.
No comments:
Post a Comment