Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, June 25, 2012

SHABIKI WA KICHINA AFARIKI KWA KUTOLALA SIKU 11 AKIANGALIA EURO 2012


Hii ndio ilikuwa mechi ya mwisho kuiona Italy vs Ireland
Kuangalia kila dakika ya michuano mikubwa ya soka ni tamanio la kila shabiki wa dhati wa soka, lakini kuendekeza sana kiasi cha kusahau japo kulala kunaweza kukaleta matokeo mabaya.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka kijiji cha Hunan China, shabiki aitwaye Jiang Xiaoshan amekutwa amekufa baada ya kukaa macho usiku kucha kwa siku 11 huku akiangalia Euro 2012 marathon. Mechi za Euro zimekuwa zikianza 2.45 a.m kwa muda wa China, hivyo Mr.Jiang alikuwa akiangalia mechi mpaka asubuhi na baada ya hapo alikuwa akienda kazini kufanya kazi siku nzima. Kwa bahati, gazeti la Telegraph linaripoti kwamba staili ya mchina huyu imeishia kwenye balaa.

"Kijana huyo mwenye miaka 26, alikutwa amefariki na mama yake baada ya kushindwa kulala kwa siku 11 akiangalia soka, na hatimaye mambo yakawa magumu siku ambayo Italia walishinda 2-0 dhidi ya Ireland.

"Tulikuwa tunapumzika kidogo lakini siku zote tulikuwa tunaangalia soka bila kukosa mechi yoyote," rafiki mmoja alisema.

Shabiki huyo ambaye alikuwa na afya njema, lakini mfumo wa kinga yake ya mwili uliodhohofika kutokana kutopumzisha mwili kwa kulala na tabia ya kuvuta na kunywa sana pombe wakati akiangalia mechi.

Marehemu Mr.Jiang aliangalia zaidi ya dakika 1,890 za mechi na kuona magoli 51 yakifungwa. Pia inasemekana alikuwa akiisapoti England na Ufaransa kwenye michuano hiyo.

                                  SOURCE SHAFFIH DAUDA

1 comment:

  1. http://tzexim.ucoz.com/news/we_are_exporters_of_dried_fruits_nuts_and_cereals/2012-06-25-1

    ReplyDelete