WATU
88 wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani hapa kwa kuhusika na matukio
mbalimbali ya uharifu ikiwemo wizi wa mafuta aina ya diseli kwaajili ya
kuendeshea mitambo katika ujenzi wa barabara kati ya
Tunduma-Sumbawanga.
Kamanda
wa polisi mkoani Mbeya Athuman Diwani alisema watuhumiwa wa makosa hayo
wamekamatwa katika oparesheni maalumu ya kupambana na uharifu iliyoanza
Juni 8 mwaka huu.
Kamanda
Amesema katika matukio ya wizi wa diseli jumla ya lita 4,440 zenye
thamani ya zaidi ya shilingi laki tisa zilikamatwa na tayari mahakama
imeamuru mafuta hayo yarejeshwe yalikoibwa ili yakaendeleze shughuli za
ujenzi wa barabara huku watuhumiwa nane wa wizi huo wakiwa tayari
wamefikishwa mahakamani.
Amewataja
watuhumiwa hao kuwa ni Lusekelo Paza,Anyemike Swile,Weiti
Mwakatumbula,Michael Mwampamba,Mahona John,Erasto Mwaipaja,Seleman
Nasoro na Hassan mrisho.
Amesema
katika oparesheni hiyo pia zimekamatwa pikipiki tatu zilizoibwa
akizitaja kuwa ni yenye namba T 584 BPU aina ya Star,T 301 BRU aina ya
SanLG na T 489 BQU aina ya Sanya.
Mali
nyingine ni bunduki mbili zilizotengenezwa kienyeji zinazotumia risasi
za Shotgu,risasi nane,Televisheni mbili,kompyuta ndogo(Laptop)
mbili,Printa moja,redio tatu,mbili aina ya Sub ufa na moja ya kawaida
pamoja na simu nane za aina mbalimbali.
Hata
hivyo amesema matokeo hayo mazuri yanatokana na ushirikiano mzuri
ulioneshwa kati ya raia wema na askari wa jeshi hilo akisema wananchi
walijitahidi kwa kiasi kikubwa kutoa taarifa juu ya uwepo wa vitendo vya
uharifu.
Amewaomba
wananchi kuendeleza ushirikiano huo mzuri akisema utasaidia kwa kiasi
kikubwa kupunguza uharifu na kuufanya mkoa kuwa na amani na utulivu.SOURCE MBEYA YETU | |
No comments:
Post a Comment