Baada
ya kusumbuliwa kwa kipindi kirefu kwa ugonjwa ambao ulisababishwa na
uvimbe tumboni hatimaye mwigizaji machachari kabisa kunakoulingo wa
filamu hapa nchini Juma Kilowoko maarufu kwa jina la Sajuki amerejea
nchini siku kadhaa zilizopita. Akiwa anazungumza na waandishi wa
Globalpublishers Sajuki alidai kwa sasa hali yake imerejea kama zamani
na anawashukuru Watanzania wote waliomchangia kwa hali na mali
kufanikisha matibabu yake na anathamini mchango wao, bila kuwafumbia
macho waliokuwa wanazungumza yasiyokuwepo Sajuki hakuacha kuzungumzia
waliomzushia kifo na kusema kuwa yeye hana kinyongo na
mtu na Mungu awabariki. Pichani ni sajuki baada ya kurejea kutoka India alikokwenda kwa matibabu.
APRM YAKUTANA NA VIONGOZI WA WANAFUNZI KUJADILI NAFASI YA VIJANA KATIKA
UTAWALA BORA
-
Katibu Mtendaji wa Mpango wa Hiari wa Nchi za Umoja wa Afrika wa
Kujitathmini kwa Vigezo vya Utawala Bora (APRM) Tanzania, Bw. Lamau Mpolo,
amekutana na...
3 hours ago

No comments:
Post a Comment