Hili ndilo basi la Tony Sley ambalo limepata ajali jana usiku na kuua watu watatu na kujeruhi 38
Basi la Tony Sley
Majeruhi wakisubiri matibabu Hospitali ya mkoa wa Iringa.
Majeruhi
wa basi la Tony Sley Bi Agnesy Lukasi akiwa na mtoto wake Dina Lukasi
(4) wakisubiri kupewa matibabu katika Hospital ya mkoa wa Iringa baada
ya kufikishwa hapo usiku huu wakitokea eneo la ajali mlima wa Kitonga
Ajali ya
basi ya Tony Sley yenye namba za usajili T 218 ACH lililokuwa
likitokea Tunduma mkoani Mbeya
kwenda jijiniD’Salaam imeua watu watatu wakiwemo wawili raia ya Zambia
na mmoja mtanzania na kujeruhi wengine 38.
Ajali hiyo imetokea
katika eneo la kona za mlima wa kitonga kwenye barabara kuu ya Iringa
–D’Salaam jana majira yasaa 12 za jioni baada ya dereva wa basi
hilo kushindwa kulipita lori lilolokuwa mbele yake.
Wakizungumza
katika eneo hilo na Hospitali ya mkoa wa Iringa majeruhi wa
ajali hiyo waliolazwa katika hospitali yawilaya ya Kilolo
Ilula walisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wao
alisema Agnes Lukasi (30).
Agnesy alisema
kuwa kwa upande wake alikuwa amekaa siti ya mbele na wakati dereva huyo
akifanya uzembe huyowalikuwa wakimshuhudia hata kujaribu kumuonya bila
mafanikio.
Alisema kuwa katika basi hilo alikuwa na mtoto wake Dina Lukas (4) ambaye pia amejeruhiwa katika paji lake la uso.
Kamanda wa polisi wa
mkoa wa Iringa Michael Kamhanda ambaye alifika eneo la tukio pamoja na
mkuu wa kikosi chausalama barabarani mkoa wa
Iringa aliuthibitishia mtandao huu kuwa jumla ya abiria
38 ndio waliojeruhiwa katika ajalihiyo.
Aliwataja baadhi
ya majeruhi ambao majina yao yamepatikana na kulazwa katika hospital
teuli ya mkoa wa Iringa kuwa ni pamoja na Boyd Simwings(43) , Violet
Chambale(35),Zilombo Wake(38),Warmen Mambwe (33),Eugen Maluge(39),
Mwamba Andrew (27) , Bright Mwalukanga (33) na John Lemba( 30) wote raia
wa Zambia.
Wengine ni Martine Shombe(
29) mkazi wa Tunduma, Zainabu Amuri (32) mkazi wa D’Salaam , Efrain
Mwampashi (31) mkazi wa Tunduma, Sebastian Mhaya(25) mkazi wa Tunduma,
Vedastus Benjamin (11) mkazi wa Tunduma, Mrashi Handu (38) mkazi wa
Igulusi, Juma Ramadhan (40) mkazi wa Tunduma, Twaribu Juhim (39) mkazi
wa Arusha, Muka Muka (26) mkazi wa Tunduma, Edina Ramadhan (3)
mkazi wa Tunduma na Benjamin Enock (33) mkazi wa Mbeya.
Wengine
ni Agness Lukas (30) mkazi wa Tunduma , Dina Lukas (4) mkazi wa Tunduma
Beatrice Msakanti( 42) mkazi wa Zambia, Besa Shadrack (32) mkazi wa
Zambia na Mary Mumba (48) mkazi wa Zambia pia.
Alisema majina
ya majeruhi zaidi yatapatikana hivi karibuni baada ya majeruhi waliopo
Hospital ya wilaya ya Kilolo Ilula kufika mjini Iringa.
Mbali
ya majeruhi hao pia aliwataja waliopoteza maisha katika ajali hiyo kuwa
ni Cla Pily (32) na Dany Kawina (43)
wotewafanyabiashara raia wa Zambia pamoja na Abel Nelson (32) ambaye ni
mtanzania.
Kamanda
Kamhanda mbali ya kueleza masikitiko yake juu ya ajali hiyo bado
aliwaonya madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani na
kuendesha kwa uangalifu wa hali ya juu na kuwa jeshi lake mkoani Iringa
halitalala kuwabana madereva wazembe. Chanzo: www.francisgodwin.blogspot.com
No comments:
Post a Comment