Muda mfupi
baada ya Boca Juniors kufungwa na Corinthians kwenye fainali ya Copa
Libertadores, kiungo wa miaka 34, Juan Roman Riquelme alitangaza nia
yake ya kuondoka kwenye klabu hiyo kwa mara ya pili. Ilikuwa habari
mbaya sana kwa mashabiki wa Boca Juniors ambao walipata taarifa kwamba
shujaa wao anapanda ndege ndege kuelekea Brazil kujiunga na Flamengo.
Hivyo
huku Riquelme akijiandaa kuondoka, kama alivyofanya mwaka 2002
alipojiunga na Barcelona, maelfu ya mashabiki wa Boca waliungana mitaani
kuandamana kwenye miji tofauti nchini Argentina kumuomba Riquelme
asiondoke.Mkusanyiko mkubwa zaidi uliwahusisha mashabiki takribani 5000
pale La Bombonera mjini Buenos Aires, ambapo mashabiki hao walikusanyana
mitaani mpaka kwenye uwanja huo. Kwa mujibu wa Ole, klabu hiyo mwanzoni
walisema hawatowaruhusu kuingia uwanjani kwa kuwa hakukuwa na ulinzi,
lakini baadae waliwaachia washabiki kuingia uwanjani huku wakiwa mabango
ya kumuomba mchezaji wao kipenzi asiondoke huku wangine wakiimba
"Riquelme ni Boca, Boca haondoki!"
Jambo kama hili lilishawahi kutokea jijni London wakati Manuel Almunia alipoondoka Arsenal.
Kwa
ujumla, Riquelme amekaa miaka 12 na Boca Juniors, akicheza mechi zaidi
ya 300, akishinda makombe matano ya Primera Division na makombe matatu
ya Copa Libertadores. Alikuwa mchezaji bora wa Argentina kwa misimu
minne.
No comments:
Post a Comment