Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, July 10, 2012

DAWA ZA ARV ZASAIDIA KUPUNGUZA IDADI YA MAAMBUKIZI YA UKIMWI.



NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE-ARUSHA

MATUMIZI ya dawa za kurefusha maisha kwa watu wenye ugonjwa wa Ukimwi nchini ,ARVS,sanjari na elimu inayotolewa ya kupambana na maambukizi ya Ukimwi,yamepunguza idadi ya vifo vinavyotokana na Ugonjwa wa Ukimwi na kuwawezesha kushiriki katika shughuli zao za kujipatia vipato na kuongeza tija katika shughuli zao za kila siku .

Hayo yameelezwa na Daktari  Twaha Ahmed, alipokuwa akitoa mada kwenye semina ya mafunzo elekezi kwa wanahabari kuhusu maambukizi yaVirusi vya ugonjwa wa  Ukimwi na kueleza kuwa matumizi hayo yamekuwa na faida kubwa kwa wananchi ambao wameshaathirika na sasa wanaendelea kutumia dawa hizo za kurefusha maisha.
Dakta, Twaha, ambae ni mshauri wa maswala ya afya ya binadamu katika mashirika na taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa ,ametolea mfano wa nchi ya Brazil ,barani Amerika ya kusini, kuwa ni ya mfano kutokana na wananchi wake ambao wameathirika na Ukimwi wamekuwa wakitumia dawa hizo za ARVS kwa ajili ya kurefusha maisha bila kuachia njiani na sasa wanaendelea vizuri  na wanashiriki katika shughuli za uzalishaji mali.
Amesema hali hiyo ya matumizi ya dawa nchini Brazil, ni tofauti na hapa nchini ambapo   baadhi ya wagonjwa wa Ukimwi, wamekuwa wakikatisha  matumizi ya dawa hizo za ARVS, kutokana na kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu matumizi ya dawa hizo ,kukata tamaa, na matokeo yake kupoteza maish na wengine kuendelea kudhoofika na kushindwa kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji mali

No comments:

Post a Comment