Mwanamuziki mahili wa miondoko ya hip hop nchini maarufu kwa jina la Izzo Bizness kutoka mkoa wa Mbeya ametamka rasmi kupitia ukurasa wa facebook na kwa njia ya mawasiliano ya messeji na Dj sek kuwa leo tarehe 31/07/2012 anatarajia kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la "UTARUDISHWA" ambapo humo ndani amemshirikisha msanii mkali wa RnB Belle 9.
Ngoma hiyo inafuata baada ya kuachia video yake ya "Nakuchukia Mwaka Jana" na Imefanyika kwa kushirikiana na studio za Dirty Mode Records chini ya Produer mahili nchini Tanzania, Producer Triss. Izzo alisema kuwa ngoma hiyo ambayo anaamini itakuwa gumzo sana kwa watanzania kutokana na ilivyokuwa ya kitofauti itakuwa hewani kupitia vituo mbalimbali vya radio kuanzia kesho siku ya Jumanne.
"Watanzania Tunaomba Ushirikiano wenu wa dhati ku-support kazi hii pia kuona namna gani Dirty Mode inakubalika na kupewa nafasi ya kufanya kazi na wasanii wakubwa nchini na hata nje ya Nchi".
ILA NYIE CCM NI NOMA SANA, YAANI UBAYA UBWELA
-
Na Said Mwishehe,Michuzi TV
NILIKUWA Najiongelesha tu kichwani kuhusu hii CCM basi nikajikuta nacheka
tu,ndio kununa siwezi. CCM kwa jinsi walivyo hawa ...
2 hours ago
No comments:
Post a Comment