Hali ni tete Mjini Unguja baada ya kundi la Uamsho kuamua kuwaombea Dua
waliozama na Meli, lakini habari toka kwa mtu ambae yupo huko anasema
askari wameenda na kuwatawanya kwa mabomu, habari zaidi tutawajulisha
muda si mrefu.
HABARI ZAIDI ZITAWAJIA MDA SI MREFU
Jeshi
la Polisi Zanzibar limelazimika kutumia Mabomu ya Machozi ili
kuwatawanya wafuasi wa kikundi cha Uamsho waliokuwa wamekusanyika
kufanya Dua ya kuwaombea watu waliokufa katika ajali ya kuzama kwa Meli
ya Mv. Skagit katika Mitaa ya Mbuyuni.
Habari kutoka Zanzibar zinadai kuwa Jeshi hilo la Polisi lililazimika kutumia Mabomu ya Machozi kutokana na kikundi hicho cha Uamsho kuanza kuhubiri siasa badala ya kufanya Dua hatua iliyosabaisha kuvunjika kwa amani katika mitaa hiyo.
Mwandishi wa Kituo hiki cha Uhuru FM aliyeko Mjini Zanzibar amesema licha ya Watanzania kuendelea kuomboleza vifo vya watu waliokufa katika ajali hiyo, bado kikundi hicho cha Uamusho kimeendelea kufanya sisasa badala ya kufanya Dua.
Pia imeelezwa kuwa chanzo cha Mabomu hayo ya Machozi ni kikundi hicho kufanya Dua yenye utata huku masuala ya siasa yakijitokeza hatua iliyopelekea kuwepo kwa vurugu za hapa na pale hivyo Jeshi likaamua kutumia nguvu ya ziada ili kuwatawanya.

chanzo-hansbaby
No comments:
Post a Comment