Watu
wapatao 35 wamekufa kufuatia mafuriko yaliyotokea katikati mwa Nigeria
baada ya mvua kubwa na kusababisha bwawa kufurika karibu na mji wa Jos.
Msemaji
wa shirika la msalaba mwekundu katika eneo hilo amesema nyumba zipatazo
mia mbili, nyingi zikiwa zimejengwa kwa udongo zimezama au kuharibiwa
na mafuriko.
Shirika
la Taifa la Kushughulikia Majanga limeanza operesheni ya misaada ya
dharura.Maafisa wanasema watu wapatao ishirini na watano hawajulikani
walipo na kwamba idadi ya watu waliokufa inatarajiwa kuongezeka.
Mtu mmoja alinukuliwa akisema kuwa amewapoteza watoto wake saba katika mkasa huo.
Msemaji wa shirika la msalaba mwekundu katika Jimbo la Plateau amesema miongoni mwa waliofariki ni mzee wa miaka 90
No comments:
Post a Comment