Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, August 1, 2012

MANCHESTER WAPATA UDHAMINI MPYA WA JEZI - IJUE LISTI YA VILABU VYENYE MIKATABA MINONO YA JEZI


Manchester United leo wametangaza kwamba Chevrolet watakuwa wadhamini wao wapya wa jezi, huku kampuni hiyo kubwa ya kutengeneza magari kutoka Marekani wakijipanga kuanza kuweka jina lao kwenye jezi za United kuanzia msimu wa 2014/15.

Kiasi gani kampuni hiyo inayomilikiwa na General Motors imeilipa United kwa mkataba wa miaka saba imebaki kuwa siri, lakini inategemewa kuwa imezidi kiasi cha £20 million ambacho United wanalipwa sasa hivi na kampuni ya Bima ya AON.

Udhamini wa jezi ya Liverpool na Standard Chartered pamoja na wa Manchester City na Etihad nao wanalipwa £20million kwa mwaka, huku Sunderland nao wakitegemewa kuingia kwenye nafasi za juu baada ya kusaini dili la udhamini na Invest Africa.

Klabu ya Barcelona ambayo miaka iliyopita ilikuwa haina utamaduni kuvaa jezi zikiwa na nembo ya mdhamini kwenye kifua  ndio wanaongoza sasa kwa kuwa na mkataba mnono wenye thamani ya £25million kwa mwaka.

Wajerumani Bayern Munich wanafuatia kwa kuwa wanalipwa na Deutche Telecom  £23million kwa mwaka kwa udhamini wa jezi.

hii ndio listi kamili ya vilabu vyenye mikataba minono ya jezi.

1. Barcelona - £25m-a-year (Qatar Foundation)
2. Bayern Munich - £23.6m-a-year (Deutche Telekom)
3. Manchester United - £20m-a-year (Aon)
3. Liverpool - £20m-a-year (Standard Chartered)
3. Manchester City - £20m-a-year (Etihad Airways)
3. Sunderland - £20m-a-year (Invest in Africa)
7. Real Madrid - £16.8m-a-year (Bwin)
8. Chelsea - £13.8m-a-year (Samsung)
9. Tottenham Hotspur - £10m-a-year (Autonomy & Investec)
9. AC Milan - £10m-a-year (Emirates)
9. Newcastle United - £10m-a-year (Virgin Money)

No comments:

Post a Comment