Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, July 22, 2012

Mvua na dhoruba yaleta mafuriko Beijing



Mafuriko mjini Baijing
Mji Mkuu wa Uchina, Beijing, umepata mvua kubwa kabisa kuwahi kutokea kwa zaidi ya miaka 60.
Mvua kubwa ya jana ilifurika mabara-barani, kupeperusha mapaa, na kuporomosha miti na milingoti ya taa.Watu kama 10 wamekufa, na maelfu wamehamishwa makwao.
Maji mjini yalikuwa yanafika kiunoni.
Safari za ndege zaidi ya mia mbili zilivunjwa, na hivo kuwaacha maelfu ya watu wamenasa kwenye viwanja vya ndege.
Mvua sasa imeanuka mjini Beijing, lakini mvua kubwa inatarajiwa kaskazini-mashariki na kusini-magharibi mwa Uchina.

No comments:

Post a Comment