Mwanahabari maarufu ambaye pia ni mwandishi wa Blogi amefungwa jela
miaka 18 nchini Ethiopia kwa madai ya kukiuka sheria ya ugaidi.
Eskinder Nega na wenzake 23 walipatikana na hatia mwezi uliopita.
Serikali ya Ethiopia inadai kuwa kundi hilo ni la kigaidi.Walikamatwa kwa madai ya kuwa na uhusiano na kundi moja la upinzani lililo na makao yake Marekani kwa jina Ginbot Seven.
Mahakama hiyo ya Addis Ababa pia ilimfunga jela maisha mwanaharakati wa upinzani,Andualem Arage.
Kutokana na kazi yake ya uwana-habari na kuandika Blogi, Mwezi wa
May, Eskinder alipewa tuzo maarufu la kimarekani la Pen America's
Freedom to Write.
Makundi ya kutetea haki za kibinadamu zimekuwa ikiilaumu serikali kwa
kubuni sheria hiyo ya kukabiliana na ugaidi yakisema sheria hiyo
haifai.
Siku ya Ijumaa Mwanahabari ,Eskinder na mwanachama wa chama cha
upinzani cha Unity for Democracy and Justice party walikuwa mahakamani
kuhukumiwa.
Washukiwa wengine 16 waliopatikana na hatia mwezi wa Juni wako ukimbizini.
Walipokuwa wakiingia mahakamani wawili hao waliwapungia mikono jamaa
zao na marafiki pamoja na maafisa wa kibalozi waliokuwemo ndani.
Eskinder alikamatwa mwezi wa Septemba mwaka jana baada ya kuandika
makala iliyokuwa ikiilaumu serikali ya Ethiopia kwa kukamata wapinzani
wake kwa kutumia sheria ya ugaidi.
Miongoni mwa watu ambao wamekamatwa chini ya sheria hiyo ni msanii na
mcheza filamu maarufu nchini Ethiopia, Debebe Eshetu ambaye ni mkosoaji
mkuu wa serikal
No comments:
Post a Comment