Kamanda
wa polisi mkoa wa Singida,Linus Vicent Sinzumwa akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) juu ya mauaji yaliyofanywa na
wafuasi wa CHADEMA. (Picha na Nathaniel Limu).
Jeshi
la polisi mkoa wa Singida, linawashikilia wakazi 18 wa kata ya Ndago
jimbo la Iramba magharibi,kwa tuhuma ya kumuua mwenyekiti wa umoja wa
vijana CCM (UVCCM),Yohana Mpinga (30) baada ya kumpiga kwa kutumia
silaha za jadi.
Kamanda
wa Jeshi la polisi mkoa wa Singida, Linus Vicent Sinzumwa alisema tukio
hilo la kusikitisha limetokea julai 14 mwaka huu saa kumi alasiri huko
katika kijiji cha Ndago.
Alisema
siku ya tukio,Chama Cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA) kilikuwa na
kibali halali cha kufanya mkutano wa hadhara katika kijiji hicho cha
Ndago na mgeni rasmi katika mkutano huo,alikuwa mbunge wa jimbo la
Ubungo jijini Dar-es-salaam.
Sinzumwa
alisema mara baada ya CHADEMA kuanza mkutano huo,viongozi wake walianza
kuporomosha mvua ya kashifa mbalimbali dhidi ya mbunge wa jimbo hilo
Mwingullu Nchemba, kitendo ambacho kiliudhi baadha ya watu waliokuwa
wamehudhuria mkutano huo.
“Wananchi
hao ambao walichukizwa na kitendo cha kukashifiwa mbunge wao,walianza
kupiga kelele kuwa hawataki mbunge wao akashifiwe na badala yake
wanataka kusikia sera za CHADEMA tu na si vinginevyo.Hata hivyo,viongozi
hao waliendelea tu kuporomosha kashifa dhidi ya Mwingullu na
kusababisha kuanza kwa vurugu”,alisema.
Kamanda
huyo alisema kuwa vurugu hizo zilihusisha kundi la wanachama wa CHADEMA
na wa CCM na zilisambaa.Wanachama hao walianza kurusha mawe ovyo na
askari wachache wa polisi waliokuwepo,walizidiwa nguvu na makundi hayo.
“Huyu
mwenyekiti wa vijana CCM Yohana,yeye akikimbilia kwenye nyumba ya
mwalimu Shume Manase Mpinga ili kuokoa maisha yake,lakini kundi la
wananchama wa CHADEMA wakiwa wamebeba fimbo na mawe,walimpiga sehemu
mbalimbali za mwili wake na kusbabisha kifo chake papo hapo”,alisema
kamanda Sinzumwa kwa masikitiko makubwa.
SOURCE MO BLOG
No comments:
Post a Comment