Kocha wa Yanga, Tom Saintfiet |
Na Prince Akbar
PIGO Yanga. Wachezaji watatu tegemeo wa klabu hiyo ni
majeruhi na hawatacheza mechi ya kesho dhidi ya Waw Salaam ya Sudan Kusini
katika klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
Akina nani hao? Ni kipa Ally Mustafa Barthez, beki Juma
Abdul na kiungo Haruna Niyonzima kutoka Rwanda.
Nani kasema? Ni kocha Mkuu wa Yanga, Mbelgiji Tom Saintfiet
alipozungumza na BIN ZUBEIRY mchana wa leo juu ya maendeleo ya kambi yake.
Mtakatifu Tom amesema anasikitika mno alipanga kumuanzisha
Barthez katika mechi tya kesho, lakini kwa kuwa ameumia sasa atalazimika kuanza
Mghana Yaw Berko tena aliyetunguliwa mawili, Yangva ikilala 2-0 mbele ya
Atletico FC ya Burundi juzi.
Tom amethibitisha watatu hao wote, Barthez, Juma Abdul na
Haruna hawatapewa jezi kwenye mechi ya kesho kwa kuwa wanaendelea na tiba na
hata leo wameshindwa kabisa mazoezi.
Sasa Yanga inabakiwa na wachezaji 17 walio fiti, ambao ni kipa; Yaw Berko, mabeki;, David Luhende, Kelvin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’,
Godfrey Taita, Ladislaus Mbogo, Oscar Joshua na Stefano Mwasyika, viungo; Athumani Iddi ‘Chuji’, Rashid
Gumbo, Juma Seif ‘Kijiko’, Shamte Ally, Nizar Khalfan na Idrisa Assenga na washambuliaji; Said Bahanuzi, Hamisi
Kiiza na Jerry Tegete.
Yanga inahitaji lazima kushinda mechi ya kesho,
ili kufufua matumaini ya kutetea ubingwa wao, baada ya juzi kuanza vibaya kwa
kuchapwa 2-0 na Atletico.Kikosi cha Yanga, Barthez wa kwanza kulia waliosimama na Juma Abdul ni wa katikati walioinama.SOURCE http://bongostaz.blogspot.com/ |
No comments:
Post a Comment