MWENYEKITI wa Chama cha
Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba ameitaka Serikali kuzingatia hoja
mbalimbali za waislamu katika mchakato wa katiba mpya ili kumaliza zoezi hili
kwa wakati.
Amesema kutokana na
kutosikilizwa kwa waislamu kuhusu hoja zao dhidi ya uundwaji wa katiba mpya ni
kikwazo cha utekelezaji wa zoezi hilo linalotarajiwa kufikia tamati Aprili 26 mwaka 2014.
Profesa Lipumba alikuwa
akihutubia Kongamano la Waislamu jijini hapa lililoandaliwa na Jukwaa la Katiba
Mkoa wa Arusha juzi na kuhadharisha kuwa iwapo hoja hizo hazitazingatiwa
itakuwa vigumu kukamilika kwake.
“Mchakato wa Katiba Mpya sasa
ni miezi 16 na iunatarajiwa kukamilika Aprili 26 mwaka 2014, ni wazi iwapo
zoezi litaendelea kukumbwa na malalamiko kama haya ya waislamu itakuwa vigumu
kukamilika kwa wakati, na iwapo litakamilika basi hiyo haitakuwa katiba
iliyokamilika kwakuwa haitoshelezi mawazp na maoni ya wananchi”
Alisema.
Alisema.
Hata hivyo aliwataka wananchi
kuhakikisha wanajitosa katika mchakato wa kutoa maoni bila kukosa ikibidi kwa
kurikodi kile wanachokipendekeza ili katiba hiyo itakapokamilika waione iwapo
inayo maoni waliyotoa ama maoni hao hayapo waikatae.
Alisema mchakato wa kudia
kuwepo kwa katiba mpya kulianza miaka ya tisini kupitia chama chake, na hata
mwaka 2001 walivamiwa na Polisi wakiwa katika maandamano ya amani wakidai
katiba mpya na tume huru ya uchaguzi ambapo alivunjwa mkono na kuporwa saa yake
na Polisi.
No comments:
Post a Comment