Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, July 18, 2012

RAIS JAKAYA KIKWETE ATAKA RASILIMALI ZA KUPAMBANA NA MALARIA




Rais Jakaya Kikwete akiongea na vyombo vya habari leo mara baada ya kufungua rasmi ofisi za Ofisi za  Umoja  wa Viongozi wa Afrika  wa Kudhibiti Malaria(ALMA) iliyopo katika Kituo cha Mkakati wa Kupambana na Malaria(Ceemi), jijini Dares Salaam akishirikiana na mgeni wake Rais wa Liberia Ellen Sirleaf Johnson leo.


NA MAGRETH KINABO – MAELEZO

RAIS wa Liberia, Ellen  John-son Sirleaf amewataka viongozi wa  nchi za Afrika kufanya jitihada za kuhakikisha wanatenga rasilimali za kutosha za  kuweza kupambana na ugonjwa wa Malaria ili   ifikapo mwaka 2015 Bara la Afrika lifanikiwe kutokomeza ugonjwa huo kwa asilimia zero.

Kauli hiyo ilitolewa leo na Rais  huyo wakati  wa sherehe za uzinduzi wa Ofisi za  Umoja  wa Viongozi wa Afrika  wa Kudhibiti Malaria(ALMA) iliyopo katika Kituo cha Mkakati wa Kupambana na Malaria(Ceemi), jijini Dares Salaam.
Alisema lengo kubwa la ALMA ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2015 Bara la Afrika linaondokana  na ugonjwa huo ikiwemo  vifo vinavyosababishwa na  Malaria .

“Tunaweza kufanya hivyo ili tuweza kufanya tunatakiwa kuchukua hatua  za kuwa na rasilimali za kutosha na kuzitawanya katika vituo vya afya kama ilivyo katika azimio letu la Abuja.” Alisema Rais Hellen.

Aliongeza kuwa  jitihada  hizo zitafanikiwa kwa kuboresha usimamizi bora  wa mfumo wa  fedha ili kuweza kukabiliana na tatizo la uhaba wa fedha kiasi cha   dola za Marekani  bilioni  3.2 .

No comments:

Post a Comment