Samatta. Picha ta Maktaba |
Mshambuliaji
chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ‘Sama Goal’,
leo ametoa pasi zote za mabao mawili ya klabu yake, Tout Puissant
Mazembe, kwenye Uwanja wa TP Mazembe mjini Lubumbashi katika mchezo wa
Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Berekum Chelsea ya Ghana, uliomalizika
hivi punde kwa sare ya 2-2.
Mapande
yote ya Samatta leo yalitumiwa vema na Tressor Mputu Mabi katika dakika
za 11 na 32 kuipatia mabao Mazembe, wakati Chelsea ya Ghana ilionyesha
yenyewe ni moto kweli kwa kupata sare Lubumbashi. Mabao ya Chelsea
yalifungwa na Emmanuel Atukwei Clottey katika dakika za 71 na 84. Dakika
ya 75, Samatta alimpisha Francis Kasonde wakati huo wenyeji wakiwa
wanangoza 2-1, lakini kutoka kwake kulisababisha jahazi kuzama kabisa.
Katika
mchezo wa kwanza, Mazembe ilifungwa 1-0 wiki iliyopita, Samatta
akifunga bao la kufutia machozi Cairo na sasa mabingwa hao mara nne
Afrika wana pointi moja tu ndani ya mechi mbili, kuashiria kwamba wana
kibarua kizito kutimiza ndoto zao za kutwaa ndoo ya tano Afrika.
Mechi
nyingine ya Kundi lao, itafuatia saa 5:00 usiku, kati ya wapinzani wa
jadi katika soka ya Misri, Zamalek na Al Ahly. na bin zubeiry
No comments:
Post a Comment