
Miss Moro Morogoro 2012 Joyce Baluhi katikati akiwa na washindi
wenzake, Salvina Kibona mshindi namba kushoto na Irene Thomas mshindi
namba tatu mara baada ya kumalizika kwa shindano la Miss Morogoro
lililofanyika katika hoteli ya Morogoro Hoteli mwishoni mwa wiki mkoani
hapa.

Miss Moro Morogoro 2012 Joyce Baluhi kushoto akiwa na Miss Morogoro 20111, Asha Salehe kulia mara baada ya kumkabidhi taji hilo.

Mgeni rasmi shindano la Miss
Morogoro 2012 ambaye ni Afisa Mwendeshaji wa mfuko wa pensheni kanda ya
mashariki na kati (PPF) Astronaut Liganga kulia liyesimama akiwa katika
picha ya pamoja na Miss Morogoro 2012, Joyce Baluhi aliyekaa, Mratibu wa
shindano hilo Frank Kikambako kushoto aliyesimama na warembo wengine
walioingia tano bora mara baada ya kutangazwa matokeo na kuwapata
washindi.

Hawa ndiyo warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bara kutoka na
kuchujwa kupata mshindi wa kwanza, pili na tatu ambao warembo hao
watashiriki shindano la Miss Kanda ya Mashariki.

Picha ya pamoja ya washiriki wote 13 ambao walishiriki shindano
hilo baada ya kupanda kujukwaani na vazi la ubunifu, ufukweni na jioni
katika kinyang'anyiro hicho.

mrembu naye akiwa katika vazi la ubunifu.
Mrembo Prisca Mengi (18) akipita mbele ya majaji na mashaki na vazi la ubunifu.
Rais wa bende ya FM Academia (wazee
wa Ngwasuma), Nyoshi El- Saadat akiimba wakati bende yake ikitumbuiza
mashabiki waliohudhuria shindano hilo ndani ya viwanja vya wazi vya
hoteli ya Morogoro.
Mmoja wa wanenguaji wa bendi ya FM Adademia akicheza kwa aina mpya kwa staili ya Vundesa.
JOYCE Baluhi (22) ameibuka katika shindano la kumsaka Miss Morogoro
2012 baada ya kutwaa taji hilo lililokuwa na ushindani wa hali ya juu
lililofanyika kwenye viwanja vya wazi vya hoteli ya Morogoro mwishoni wa
wiki mkoani hapa.
Dalili za Baluhi kutwaa kwa taji hilo zilionekana mapema hasa katika
onyesho la vazi la ubunifu, ufukweni na jioni kabla ya kumalizia
kizingiti cha mawaswali na kuibua shngwe na ndelemo kutoka kwa mashabiki
waliohudhuria shindano hilo kwa kila hatua ambayo akionekana mlimbwende
huyu baada ya kulitawala jukwaa.
Katika shindano hilo ambalo lilisindikizwa na bendi ya muziki wa
dansi ya bende ya FM Academia (wazee wa Ngwasuma) chini ya Rais wao,
Nyoshi El- Saadat lilikonga nyoyo za wapenzi wa dansi na shindano hilo
ambapo walitumbuiza nyimbo mbalimbali zilizopo katika chati hivi sasa.
Mwandaaji wa shindano hilo la Miss Moro 2012, Frank Kikambako alisema
kuwa mshindi wa kwanza amejipatia sh400,000 huku mshindi wa pili
akipata sh300,000 na mshindi wa tatu akipata zawadi ya sh250,000 na
washiriki wote walioshiriki shindano hilo wakiambulia pesa ya sh50,000
kila mmoja kama kifuta jasho.
Naye mgeni rasmi katika shindano hilo Afisa Mwendeshaji wa mfuko wa
pensheni kanda ya mashariki na kati (PPF), Astronaut Liganga alisema
kuwa warembo waliofanikiwa kuingia tano bora na hatimaye kumpata Miss
Moro 2012 ambao wote watashiriki shindano la Miss Kanda ya Mashariki
kuwa na nidhamu mzuri itayochangia na sifa nyingine kuvuka vikwazo
katika shindano hilo.
Aliwataja warembo ambao walifanikiwa kutinga hatua ya tano bora ni Nafya Waziri (19) na Betina Lawurence (20).
Liganga alisema kuwa sifa pekee katika tasnia nyingi za michezo
ikiwemo na urembo ni kuwa na nidhamu mzuri na kuwataka washiriki wengi
ambao hawakupata nafasi ya kusonga mbele kuendeleza nidhamu
walioionyesha katika kambi ya Miss Morogoro.

No comments:
Post a Comment