Yusuph Manji |
Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti la Tanzania Daima, Manji
aliyetua Yanga mara ya kwanza Juni, 2006 kupitia ufadhili, alisema
anakwenda Jangwani kurejesha furaha iliyotoweka.
Manji amesema, baada ya kuwa kwake ndani ya klabu hiyo kwa miaka sita, kama mfadhili, mwanachama na mjumbe wa Bodi ya Wadhamini, amejionea na kujifunza mengi, hivyo anajua wapi pa kuanzia.
Alisema ingawa klabu hiyo inapaswa kujengewa msingi imara wa kiuchumi, lakini zawadi na faraja kubwa kwa wanachama, wapenzi na mashabiki, ni mafanikio ya uwanjani kwanza.
“Najua wengi watakuwa wamejiuliza maswali mengi, iweje nichukue fomu, kwanini nisibaki kuwa mfadhili, ninakwenda kutafuta nini, lakini si kingine, ni kuwapa Yanga furaha,” alisema Manji kwa kujiamini.
Alisema amechukua uamuzi huo mgumu baada ya kubaini hakuna njia nyingine ya kufanikisha ndoto zake za kuijenga Yanga imara kisoka na kiuchumi, isipokuwa kuingia kwenye uongozi kuonesha njia.
“Nimechukua fomu nikitaka kutimiza ndoto za kuifanya Yanga ya mfano Tanzania na Afrika kama nitapewa kura, pia sapoti baada ya kuingia madarakani nikishirikiana na wenzangu,” alisema na kuongeza:
“Nikiwa mfadhili, kuna mambo niliyapigania kwa maslahi ya Yanga bila mafanikio, nikaamua kujivua ufadhili (2009) na ujumbe wa Bodi ya Udhamini (Februari, 2011), nikibaki mwanachama tu,” alisisitiza.
Manji alisema, baada ya mambo kwenda hovyo ndani ya klabu hiyo hivi karibuni, wazee na vijana walimfuata wakimsihi arejee kwenye ufadhili, lakini akaona hilo pekee halitoshi, yatakuwa yaleyale.
Alisema, kiu ya kuwania uongozi kwa kiasi kikubwa imechagizwa na mapenzi yake makubwa kwa Yanga, hasa baada ya kuvuliwa ubingwa wa Ligi Kuu Bara na kufungwa 5-0 na Simba katika mechi ya kufunga pazia, Mei 6.
Alisema, vitu hivyo vimewanyima raha wanachama (akiwemo yeye), wapenzi na mashabiki wa soka, hivyo anaomba kura za wenzake akiwa na agenda nyingi; kubwa zaidi kurejesha furaha ya ushindi Jangwani.
Alisema, hiyo ni agenda muhimu zaidi kwa sababu, bila timu kufanya vizuri dimbani, hata mipango ya maendeleo ikiwamo uwekezaji, haitapangika, hivyo agenda yake ya kwanza ni kujenga kikosi imara cha mataji.
Manji alisema, hilo haliwezi kufanikiwa kwa maneno, bali kwa vitendo ikiwamo uwekezaji wa uhakika katika kikosi cha kwanza; kusajili nyota bora na kuwalipa vizuri tena kwa wakati, pia kuwa na kocha bora.
Alisema, baada ya kurejesha furaha kupitia ushindi, ndipo amani, utulivu na mshikanao vitakapotuama Yanga, hivyo uongozi kuanza kufikiria mipango zaidi ya maendeleo ikiwamo uwekezaji.
Alisema chini ya mazingira hayo Yanga haiwezi kufungwa 5-0 v na ikitokea hivyo tena chini ya uongozi wake, hatasubiri shinikizo v la wanachama kumng’oa, atajiweka kando mara moja.
Mbali ya Manji, wagombea wengine wa nafasi hiyo katika uchaguzi huo mdogo utakaofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam, ni Sarah Ramadhan, John Jembele na Edger Chibula.
Uchaguzi huo unafanyika kujaza nafasi sita zilizo wazi baada ya kujiuzulu kwa waliokuwa wakizishikilia kwa nyakati na sababu tofauti, hivyo uongozi huo uliochaguliwa Julai 18, 2010 kusaliwa na wajumbe wanne tu
SOURCE: Tanzania Daima
MGOMBEA nafasi ya uenyekiti katika uchaguzi mdogo wa klabu ya Yanga
utakaofanyika Julai 15, Yusuf Manji, amesema haendi Jangwani kutafuta
fedha wala umaarufu, akisema hana njaa ya vitu hivyo.Manji amesema, baada ya kuwa kwake ndani ya klabu hiyo kwa miaka sita, kama mfadhili, mwanachama na mjumbe wa Bodi ya Wadhamini, amejionea na kujifunza mengi, hivyo anajua wapi pa kuanzia.
Alisema ingawa klabu hiyo inapaswa kujengewa msingi imara wa kiuchumi, lakini zawadi na faraja kubwa kwa wanachama, wapenzi na mashabiki, ni mafanikio ya uwanjani kwanza.
“Najua wengi watakuwa wamejiuliza maswali mengi, iweje nichukue fomu, kwanini nisibaki kuwa mfadhili, ninakwenda kutafuta nini, lakini si kingine, ni kuwapa Yanga furaha,” alisema Manji kwa kujiamini.
Alisema amechukua uamuzi huo mgumu baada ya kubaini hakuna njia nyingine ya kufanikisha ndoto zake za kuijenga Yanga imara kisoka na kiuchumi, isipokuwa kuingia kwenye uongozi kuonesha njia.
“Nimechukua fomu nikitaka kutimiza ndoto za kuifanya Yanga ya mfano Tanzania na Afrika kama nitapewa kura, pia sapoti baada ya kuingia madarakani nikishirikiana na wenzangu,” alisema na kuongeza:
“Nikiwa mfadhili, kuna mambo niliyapigania kwa maslahi ya Yanga bila mafanikio, nikaamua kujivua ufadhili (2009) na ujumbe wa Bodi ya Udhamini (Februari, 2011), nikibaki mwanachama tu,” alisisitiza.
Manji alisema, baada ya mambo kwenda hovyo ndani ya klabu hiyo hivi karibuni, wazee na vijana walimfuata wakimsihi arejee kwenye ufadhili, lakini akaona hilo pekee halitoshi, yatakuwa yaleyale.
Alisema, kiu ya kuwania uongozi kwa kiasi kikubwa imechagizwa na mapenzi yake makubwa kwa Yanga, hasa baada ya kuvuliwa ubingwa wa Ligi Kuu Bara na kufungwa 5-0 na Simba katika mechi ya kufunga pazia, Mei 6.
Alisema, vitu hivyo vimewanyima raha wanachama (akiwemo yeye), wapenzi na mashabiki wa soka, hivyo anaomba kura za wenzake akiwa na agenda nyingi; kubwa zaidi kurejesha furaha ya ushindi Jangwani.
Alisema, hiyo ni agenda muhimu zaidi kwa sababu, bila timu kufanya vizuri dimbani, hata mipango ya maendeleo ikiwamo uwekezaji, haitapangika, hivyo agenda yake ya kwanza ni kujenga kikosi imara cha mataji.
Manji alisema, hilo haliwezi kufanikiwa kwa maneno, bali kwa vitendo ikiwamo uwekezaji wa uhakika katika kikosi cha kwanza; kusajili nyota bora na kuwalipa vizuri tena kwa wakati, pia kuwa na kocha bora.
Alisema, baada ya kurejesha furaha kupitia ushindi, ndipo amani, utulivu na mshikanao vitakapotuama Yanga, hivyo uongozi kuanza kufikiria mipango zaidi ya maendeleo ikiwamo uwekezaji.
Alisema chini ya mazingira hayo Yanga haiwezi kufungwa 5-0 v na ikitokea hivyo tena chini ya uongozi wake, hatasubiri shinikizo v la wanachama kumng’oa, atajiweka kando mara moja.
Mbali ya Manji, wagombea wengine wa nafasi hiyo katika uchaguzi huo mdogo utakaofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam, ni Sarah Ramadhan, John Jembele na Edger Chibula.
Uchaguzi huo unafanyika kujaza nafasi sita zilizo wazi baada ya kujiuzulu kwa waliokuwa wakizishikilia kwa nyakati na sababu tofauti, hivyo uongozi huo uliochaguliwa Julai 18, 2010 kusaliwa na wajumbe wanne tu
SOURCE: Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment