WAKATI
Uchaguzi Mkuu wa Yanga utafanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee,
Upanga mjini Dar es Salaam Julai 15, mwaka huu wagombea saba wako
hatarini kuenguliwa.
Hao ni Mgombea Uenyekiti, Sara Ramadham na Ujumbe Ramadhan Mzimba ‘Kampira’, Edgar Fongo, Abdallah Mbaraka, Mohamed Mbaraka, Ahmad Waziri Gao na Shaaban Katwila.
Kwa
nini? Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu amesema kwamba, Kamati ya
Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imeagiza wagombea hao
wawasilishe vyeti vyao halisi mbele ya Kamati ya Uchaguzi ya Yanga.
“Wanatakiwa
hadi Julai 4 wawasilishe vyeti halisi saa 10:00 jioni, na ili kuwapa
nafasi hawa kuwasilisha vyeti vyao, muda wa kuanza kampeni sasa
umesogezwa mbele hadi Julai 6,”alisema Sendeu, ambaye amedokeza pia
kocha mpya wa klabu hiyo, Mbelgiji Thom Saintfiet atawasili kesho.source
bin
No comments:
Post a Comment