BAADHI ya watu maarufu nchini
wamewataka wabunge kuacha mzaha katika kujadili mambo mazito yanayogusa maslahi
ya nchi.
Kauli
ya wananchi hao imekuja siku chache baada ya kubaini kuwepo na ushabiki wa
baadhi ya vyama ndani ya vikao vya bunge vinavyoendelea na kulisababishia
kukosa hadhi ya bunge.
Wakizungumza kwa nyakati
tofauti na FULLSHANGWEBLOG jijini Dar es Salaam jana, watu hao walisema kuna ulazima kwa
viongozi wa vyama vyote kutoa elimu kwa wabunge wao ili kuepuka vurugu
zinazotokea bungeni hivi sasa.
Miongoni mwa watu hao, ni
Mhadhiri Msaidizi Chuo Kikuu cha Dar es Slaam Bashiru Alli alisema bunge hilo
limetawaliwa na mzaha mwingi.
Alisema mambo mengi
yanayohitaji kupatiwa ufumbuzi kupitia mijadala hiyo yamekuwa hayajadiliwi kwa
kiwango cha kina kitendo kinachosababisha wananchi kukosa majibu ya kuridhisha
katika kero zao.
Alli alisema kutokana na
vitendo hivyo pengine kuna ulazima wa kupatikana mfumo mwingine wa utakao weza
kuliendesha bunge kwa heshima na maslahi ya wananchi na si vinginevyo.
Vile vile anasikitishwa na
mahudhurio ya wabunge katika vikao hivyo muhimu vinavyojadili matatizo ya
wananchi kwa madai kuwa wengine wako safarini.
Aidha, hapendezwi na vitendo
vya Kamati za Bunge Kuendelea wakati huu muhimu wa kujadili bajeti kwani kikao
hicho cha bunge kinauzito hivyo kila mbunge anapaswa kuwa bungeni.
Katibu
Mkuu wa Chama cha (NCCR) Mageuzi, Sam Ruhuza alisema anashangazwa na mfumo wa
bunge la sasa unavyoendelea kwa sababu haukidhi mahitaji ya wananchi badala
yake unaangalia ushabiki wa chama.
Aliongeza
kuwa kutokana na wabunge hao, kushindwa kuzungumzia hoja au changamoto zilizopo
katika majimbo yao na kuzitafutia ufumbuzi,kuna haja ya kupatiwa semina ya
kuwakumbusha wajibu wao wakati wakiwa bungeni.
Naye
Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT)Usharika wa Matumbi,
Christophile Kalata, alieleza kuwa watanzania walipofika sasa wanahitaji
kiongozi shupavu anayeweza kusimamia rasilimali au maendeleo ya nchi kwa
maslahi yao.
“Nchi
zilizoendelea zinapenda kuona au kushuhudia Tanzania ikikumbwa na misukosuko,
hivyo zinaweza kutumia mwanya huo kwa kuwatumia viongozi waliopo kulumbana ili
kazi za maendeleo ya nchi zisimame au zizorote” alisema Kalata.
Naye Hashim Rungwe ambaye ni
Mwanasheria aliwataka wabunge kutekeleza wajibu wao waliotumwa na wananchi
kuliko kutaka kujijengea umaarufu usiokuwa namsigi.
Alisema wabunge hawako pale
kwa lengo la kuonyeshana kuwa nani bingwa wa kusema japo anachosema hakina
maslahi na nchi.
No comments:
Post a Comment