MKUU
wa mkoa wa Katavi, Dr Rajabu Rutengwe amewataka wawekezaji
wanaokwenda kuwekeza katika sekta ya madini katika mkoa wa Katavi
wawasiliane na ofisi za serikali mkoani humo kabla ya kuingia katika
mikataba ya uendeshaji wa shughuli za uzalishaji katika maeneo husika
Mwandishi
wa habari hii kutoka Katavi Willy Sumia anaripoti kuwa wito huo
umetolewa na mkuu kufuatia utapeli waliofanyiwa wawekezaji wa kutoka
nchi ya China na kampuni yao ya Red Ore Mining Co. Ltd ya DSM na
kupelekwa eneo la pori la akiba la Luafi mpakani na hifadhi ya Taifa ya
Katavi kwa ajili ya kuendesha shughuli za uchimbaji wa madini ya chuma
na shaba.
Taarifa
zinasema kuwa kampuni hiyo yenye makao yake jijini DSM inayoendeshwa
na Raia wa nchi ya China ilianza shughuli katika eneo hilo katika
kipindi cha mwezi mmoja uliopita hadi jana walipofika askari wa
wanyamapori wa Pori la akiba la Rukwa / Lukwati/ Luafi na hifadhi ya
Taifa ya Katavi kuwaamuru waondoke katika eneo hilo kwakuwa ni eneo
lilitengwa kwa ajili ya uhifadhi wa mazingira na ustawi wa wanyama
pori.
Askari
hao walipozungumza na waandishi wa habari walisema kuwa awali
walipowakuta raia hao wa China waliweza kuwahoji na kubaini kuwa
walikuwa wameingizwa eneo hilo kimakosa na ofisi ya hifadhi hiyo
iliwaandikia barua yenye Kumb Namba RLLGR/LGR.1/72/14 ya tarehe
06/06/2012 iliyokuwa akiwapa amri ya kuondoka eneo ndani ya siku saba
tangu tarehe ya barua hiyo lakini hawakuweza kutekeleza agizo hilo
Askari
hao wa wanyamapori walisema kutokana na kushindwa kutii agizo hilo
waliamua kufika eneo husika kuwachukua viongozi wa kampuni hadi ofisi ya
Mkuu wa mkoa kwa maamuzi zaidi kwani walibaini kuwa walipewa taarifa
za uongo na mtu aliyewauzia hilo eneo kwani hilo eneo na eneo
lisilotakiwa kufanyiwa shughuli yoyote ile
Walisema
hata barua walizojibiwa na Katibu Mkuu wa wizara ya Maliasili na
Utalii yenye kumbukumbu namba HB 178/286/01/102 iliyosainiwa na ndugu
J. Muya kwa niaba ya Katibu mkuu wa wizara hiyo ya tarehe 20/06/2012
pamoja na ile iliyotoka kwa wakala wa misitu Tanzania (TFS) yenye
kumbukumbu namba TFSC.166/286/01/29 ya tarehe 25 Juni, 2012 ikieleza
kuwa eneo hilo waliloomba kwa barua siyo eneo linaloruhusiwa kwa
kufanya shughli yoyote ya kibinadamu isipokuwa kwa utafiti wa mafuta,
gesi au madini ya uraniamu tu
Akizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya kikao na Wachina wamiliki wa
Kampuni ya RedOre Mining Co. Ltd, mkuu wa mkoa wa Katavi, Dr Rajabu
Rutengwe alisema kuwa katika mazungumzo na wawekezaji hao alibaini kuwa
walitapeliwa na mtu aliyewauzia eneo hilo baada ya kuona kuwa eneo
hilo haliruhusiwi kwa shuguli yoyote.
Alisema
kutokana na hali iliyojitokeza inabidi sheria ichukue mkondo wake na
huku wawekezaji hao wakiwa nje ya hifadhi kwani tayari eneo hilo
limeshaharibiwa na kuingiza hasara kubwa Taifa hivyo ili kuepusha
malalamiko ya kuwa wageni hao wameonewa na Watanzania hivyo mahakama
ndiyo itakayoamua nani kakosea, wapi na namna gani kakosea ili kulinda
utawala bora.
Akizungumzia
juu ya aliyewatapeli wawekezaji hao mkuu wa mkoa alisema wao ndio
wanamfahamu aliyewauzia na wanafahamu watampata wapi hivyo ni jukumu la
wawekezaji kumtafuta wamuawajibishe kwa kuwatapeli ambapo mkuu huyo
wa mkoa alitoa ushauri kwa wawekezaji wengine wasiingie mkataba na
mmiliki yeyote wa ardhi katika mkoa wa Katavi bila kuwasiliana na
Halmashauri au ofisi ya madini ya kanda ya Magharibi iliyoko mjini
Mpanda kwa ushauri na msaada wa taarifa za eneo husika.
SOURCE http://kataviyetu.blogspot.com
No comments:
Post a Comment