Meli moja ya jeshi la wanamaji wa Australia imewasili katika eneo ambako meli iliyobeba wahamiaji haramu ipo.
Wakuu wa serikali ya Australia
wanasema, hali mbaya ya anga imezuia wahamiaji hao haramu kuabiri meli
hiyo ya kijeshi lakini wanamaji hao bado wanadadisi hali ilivyo.
Meli hiyo inasemekana kubeba
wahamiaji haramu kati ya 130 na 180, ilitoa ujumbe wa kutaka msaada wa
dharura wakati ilipokuwa katika eneo la bahari kati ya Indonesia na
Kisiwa cha Christmass.
Tukio hilo limejiri siku moja tu
baada ya viongozi wa mataifa hayo mawili, kuahidi kushirikiana katika
harakati za kuzuia na kuthibiti ulanguzi wa watu, baada ya meli nyingine
mbili iliyokuwa imebeba wahamiaji haramu kuzama mwezi uliopita.
No comments:
Post a Comment