Wahusika wa Matayarisho ya Mazishi ya
watu waliokuwa bado hawajatambuliwa na Jamaa zao ili kuzikwa
kiserikali wakiwa katika kazi ya kutayarisha Sanda hapo katika Viwanja
vya Maisara Zanzibar.
Madaktari wakiandika Orodha ya Maiti zinazoletwa hapo katika
Viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar Baada ya kupatikana kutoka katika
Meli ya Skagit iliozama hapo jana katika Eneo la karibu na Kisiwa cha
Chumbe Zanzibar
Baadhi ya Wananchi wakiwa wamekusanyika katika Viwanja vya
Maisara ili kuweza kupata taarifa ya Ndugu zao waliokuwa katika Meli ya
Skagit ambayo imepata Ajali ya Kuzama katika Eneo la karibu na Kisiwa
cha Chumbe Zanzibar
Baadhi ya Wageni kutoka Nchi mbalimbali wakiwa katika Viwanja vya
Maisara ili kujuwa Ndugu zao na kuangalia taratibu zinazofanyika
viwanjani hapo kutokana na Kuzama kwa meli ya skagit hapo jana katika
Eneo la karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.
Wananchi mbalimbali wakizitambua Maiti zao zilizopatikana katika
Ajali ya Meli ya skagit iliozama hapo jana katika Eneo la karibu na
Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.
Baadhi ya Maiti za
watoto zilizopatikana katika Ajali ya Meli ya Skagit iliozama zikiwa
katika Eneo la Maisara kwa ajili ya kutambuliwa na Nduguzao.Hadi
mchana huu Maiti zilizopatikana ni 39 kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi
Zanzibar na bado waokoaji wanaendelea na zoezi hilo katika eneo la
Tukio.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika Foleni ili kwenda kuzitambua
Maiti zao katika Viwanja vya Maisara kutokana na kuzama kwa Meli ya
skagit hapo jana katika Eneo la karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.Hadi
mchana huu Maiti zilizopatikana ni 39 kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi
Zanzibar na bado waokoaji wanaendelea na zoezi hilo katika eneo la
Tukio
Baadhi ya Wananchi waliozitambua maiti zao katika Viwanja vya
Maisara wakisaidiwa na Askari kutokana na Huzuni kubwa
waliokuwanazo.kwa kuzama kwa Meli ya skagit hapo jana katika Eneo la
karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.Picha Na YUSUPH SIMAI - MAELEZO ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment