Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, August 11, 2012

ALIYEJARIBU KUTAKA KUUZA MTOTO AFUNGWA JELA



Mkuu wa mkoa wa Rukwa ,Stella-Manyanya
Mkazi wa kijiji cha Ulumi tarafa ya mwimbi wilayani sumbawanga katika mkoani Rukwa Issack Lunguya (40) amehukumiwa kifungo cha miaka 2 jela ,sanjari na kulipa faini ya 2,000,000/=kwa kosa la kujalibu kumuuza mtoto wa jirani yake ili akatumikishwe kazi za ndani bila ridhaa.

Mwandishi wa habari hizi Elizabeth Ntambala anaripoti kutoka Sumbawanga kuwa ,Adhabu hiyo imetolewa katika mahakama ya Hakimu mkazi mjini Sumbawanga wakati hakimu wa mahakamani ya hakimu mkazi Rozalia Mugissa baada ya kuridhishwa na ushaidi wa upande wa mashtaka katika kesi hiyo iliyoongozwa na mwendesha mashtaka wa polisi Assistant Ispector Emmanuel Shani.

Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha mashtaka Mkaguzi Msaidizi wa Polisi
kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo 07,08 mwaka huu,amapo alikamatwa febr 21/2012 saa nne asubuhi huko ulumi alipokuwa katika harakati za kumuuza mtoto huyo mwenye umri(14)kwa mfanyabiashara mmoja ili asafirishwe kupelekwa mjini sumbawanga tayari kwa kwenda kufanya kazi za ndani.

Shani aliendelea kuileza mahakama hiyo mbele ya Hakimi Mkazi wa Rosaria Mugissa kuwa siku ya tukio mshtakiwa, kabla ya hapo kulikuwa na taarifa za siri kwamba mtuhumiwa, alikuwa akitafuta mteja wa kumuuzia mtoto huyo ambaye ni jirani yake ile hali ni yatima kwa kiasi cha 2,000,000, alimvizia binti huyo akitoka nje kwenda kujisaidia.


Aliendelea kuielezea mahaka hiyo kuwa uliandaliwa mtego kwa kumtumia mtendaji wa kijiji hicho na hatimaye mwanaume huyo akanaswa akiwa amemleta mtoto huyo sokoni huku akiwa anamdanganya kuwa anaenda kumtafutia kazi nzuri ya kuuza duka.

Hakimu Mugissa alisema kuwa ameridhishwa pasipo kuwa na shaka kwani ushahidi,watu watatu akiwamo binti huyo aliyetaka kuuzwa ambaye aliielezea mahakama kuwa yeye ni yatima na hasomi shule kutokana na kukosa mtu wa kumsomesha ikiwa kwamba siku ya tukio alirubuniwa na jirani huyo.

Alisema kutokana na shida alizokuwa nazo alilazimika kuongozana na jirani yake,mpaka walipofika kwenye nyumba moja pale ulumi alielezwa abakie nje kwanza huku yeye aingie ndani,baada ya muda mfupi alishtukia mwenyeji wake anakamatwa akiwa anapokea fedha.

Akitoa hukumu hiyo Mugissa alisema kutokana na upande wa mashtaka umethibitishwa pasipo kuacha shaka kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo kwa vile vitendo vya wananchi kuwauza,pamoja na kuwasafirisha watoto kwa lengo la kuwatumikisha kazi ngumu vimeshamiri,ile hali akititoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa mshtakiwa mwenyewe na wengine wenye tabia kama hizo tayari ameanza kutumikia kifungo kwa kukosa fedha za kulipa faini.

mwisho.

No comments:

Post a Comment