Kalala
Junior akizungumza na katika mkutano wa utambulisho kwenye ukumbi wa
MangoGarden, kulia ni kiongoz msaidizi wa Twanga Pepeta, Saleh Kupaza
huku kushoto ni Msemaji wa ASET, Mohamed Pizaro na meneja wa ASET,
Hassan Rehani.
Kalala
Junior ( Katikati) akiweka hadharani vionjo vya wimbo wake mpya,
Nyumbani ni Nyumbani kwenye mkutano na waandishi wa habari akiwa na
wanenguaji wa bendi hiyo, Frida Joseph aka Beckham, Sabrina Mathew na
Mary Hamis aka Mary Kimwana wakionyesha staili yao mpya.
Na Mwandishi wetu
UONGOZI
wa kampuni ya African Stars Entertainment Tanzania (ASET)
umemtambulisha rasmi mwanamuziki mwenye vipaji vingi, Kalala Hamza
Kalala maarufu kwa jina la Kalala Junior.
Kalala
alitambulishwa kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye
ukumbi wa Mango Garden ambapo mbali ya kusema kuwa amerejea kwa lengo
la kuendeleza bendi yake hiyo aliyokuwa nayo kabla ya kujiunga na
Mapacha Watatu.
Mwimbaji
huyo maarufu alisema kwa fumbo kuwa “Koti limembana akiwa na bendi
yake ya Mapacha na kuamua kulivua na kuacha kuendelea kulivaa tena” na
kujiunga na Twanga.
“Nimefurahi
kujiunga na Twanga tena na nimekuja na zawadi za nyimbo mbili, wimbo wa
kwanza unaitwa Nyumbani ni Nyumbani ambao kwa sasa upo katika hatua ya
mwisho na utatambulishwa rasmi wiki ijayo, ni wimbo ambao unazungumzia
mambo mbali aliyokutana nayo katika muziki mpaka kuamua kurejea
Twanga,” alisema Kalala.
Alisema
kuwa ujio wake wa Twanga siyo wa kulazimishwa, bali umetokana na
mapenzi yake mwenyewe na hasa akikumbuka fadhira za ASET ambapo ndipo
alipata umaarufu mkubwa.
“Nawaomba
wadau wa Twanga wakae mkao wa kula, kwani nimerejea kivingine na
watarajie kupata mambo mengi mazuri, nitafanya zaidi ya yale
niliyoyafanya zamani, lengo ni kuendelea kushika hatamu katika muziki wa
dansi,” alisema Kalala ambaye vionjo vyake ‘vimewashika’ mashabiki
wengi wa muziki wa dansi.
Afisa
Habari wa ASET, Mohamed Pizaro alisema kuwa ujio wa Kalala umetokana na
mpango wao waliouanzisha ujulikano Amsha Amsha Twanga Pepeta Nyumbani
ni Nyumbani .
Pizaro
alisema kuwa mpango huo ni maalum kwa kuhimarisha bendi yao na hasa kwa
wanamuziki ambao wameonyesha nidhamu nzuri wakiwa chini ya ASET na sasa
wanatumikia bendi nyingine.
Kiongozi
msaidizi wa Twanga Pepeta, Saleh Kupaza alimpokea kwa mikono miwili
mwimbaji huyo na kusema kazi ya kujihimarisha zaidi imeanza.
“Karibu
nyumbani, si unajua nyumbani ni nyumbani, tunaamini hata hao wengine
wanajifanya vichwa ngumu, nao watarejea tu,” alisema Kupaza.
No comments:
Post a Comment