MABINGWA wa 1988, Coastal Union ya Tanga wamekamilisha
usajili wa msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na wametaja kikosi
chao, kupitia facebook page yao.
Kikosi cha Coastal msimu kitaundwa na makipa; Juma Mpongo,
Abraham Chove na Rajab Kaumba, mabeki; Said Sued (Nahodha) Mbwana Kibacha (Nahodha
Msaidizi) Othman Omary, Juma Jabu, Ismail Suma, Jamal Machelenga, Cyprian
Lukindo na Philipp Mugenzi.
Viungo watakuwa ni Jerry Santo, Razack Khalfan, Mohamed
Binslum, Khamis Shango, Mohamed Issa, Mohamed Soud, Suleiman Kassim ‘Selembe’,
Lameck Dayton, Joseph Mahundi, Aziz Gilla na Shaffih Kaluani, wakati
washambuliaji ni Nsa Job, Atupele Green, Danny Lianga na Pius Kisambale.
Kikosi hicho kitakuwa chini ya Kocha Mkuu, mshambuliaji wake
wa zamani, Juma Mgunda, atakayekuwa akisaidiwa na beki wa zamani wa Pan
African, Habibu Kondo, kocha wa viungo, mchezaji wake wa zamani, Ally Jangalu
na kocha wa makipa Bakari Shime.
Msimu ujao, kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu, mkoa wa
Tanga utakuwa na timu mbili Ligi Kuu, zaidi ya Coastal nyingine ni Mgambo FC
iliyopanda msimu huu, hivyo kukumbushia enzi zile zile za African Sports ‘Wanaq
Kimanumanu’ na Wagosi hao wa Kaya.
No comments:
Post a Comment