|
CHRIS LIGHTY AKIWA NA DIDDY |
Mwanzilishi na mmiliki wa Violator Entertainment anayefahamika kwa jina
la Chris Lighty ambaye pia alikuwa mwanamuziki wa HipHop amefariki dunia
siku ya Agosti 30 huko Marekani. Chriss alifariki baada ya kujipiga
risasi ya kichwa kutokana na tafrani iliyokuwa ikimsumbua baina yake
yeye na mkewe chanzo kikiwa ni upotevu wa fedha na madeni yanayoikabili
familia hiyo, Chris ambaye alikuwa akidaiwa $5 milioni na IRS
alilazimika kuuza baadhi
ya vitu vyake ikiwa pamoja na hotel ili kuweza
kulipa deni hilo hali iliyomfanya kuonekana kama amechanganyikiwa na
muda mwingi walikuwa hawaelewani na mkewe Veronica. Chris hatasahaulika
kwa kuviinua vipaji ambavyo kwasasa ndio nguli wa muziki duniani kama
vile; 50 Cent, Maria Carey, Busta Rhymes, Diddy, Jarule na wengineo
No comments:
Post a Comment