Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, August 9, 2012

OKWI MCHEZAJI BORA 2011-2012, KAPOMBE, SARUNGI, MUCHACHO, KILOMONI NA MAFISANGO WASHINDA TUZO KWENYE SIMBA DAY - HUKU MNYAMA AKIFA 3-1



Klabu ya Simba leo imefanya tamasha lao kubwala kila mwka maarufu kama Simba Day, kama ilivyokuwa kwenye miaka mingine iliyopita klabu hiyo leo ilitoa tuzo mbalimbali kwa wachezaji wa timu hiyo pamoja na watu wengine.
Emmanuel Okwi akichkua tuzo ya mchezaji wa bora klabu kwa msimu wa 2011-2012
Kwa upande wa wachezaji Marehemu Patrick Mafisango alipewa tuzo ya heshima, Shomary Kapombe akatwaa tuzo ya mchezaji mwenye nidhamu huku talk of the town Emmanuel Okwi akichukua tuzo ya mchezaji bora wa klabu hiyo kwa msimu uliopita.

Watu wengine waliotwaa tuzo ni mwanachama wa siku nyingi wa klabu hiyo Professa Philemon Sarungi ambaye alipewa tuzo ya kuwa mtu aliyetoa mchango wa muda mrefu katika klabu hiyo, Haidari Abeid maarufu kama Muchacho aliyetwaa tuzo ya mchezaji wa bora wa Simba wa miaka ya 70's, Hamisi Kilomoni - mchezaji bora wa miaka ya 60's. Ally Sykes akapata tuzo ya heshima na udhamini.
 Katika matukio mengine timu ya klabu hiyo ilikipiga na timu ya Nairobi City Star katika mchezo wa kujipima nguvu na kujiandaa na msimu mpya unaotarajiwa kuanza hivi karibuni. Mchezo huo uliishia kwa Simba kutandikwa mabao 3-1. 
Kikosi cha Nairobi City Star waliotibua shughuli ya leo ya Simba.

Abdallah Juma, Shomary Kapombe, Emmanuel Okwi na Kanu

NA SHAFFIH

No comments:

Post a Comment