Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni Jijini Dar es Salaam
linamshilikia mfanyabishara maarufu, Marijan Abubakari maarufu kama
Papaa Msofe kwa tuhuma za mauaji. Habari zinasema kuwa Papaa Msofe
alikamatwa na Polisi juzi jijini Dar es Salaam na anashikiliwa katika
kituo cha Polisi cha Magomeni jijini humo.
Akizungumza na NIPASHE jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kinondoni, Charles Kenyela, alithibitisha Papaa Msofe kushikiliwa na
jeshi hilo kwa tuhuma za mauaji.
“Ni kweli tunamshikilia Papaa Msofe katika Kituo cha Polisi cha
Magomeni na tunaendelea kumhoji na kufanya upelelezi zaidi kuhusiana na
tukio analotuhumiwa nalo,” alisema Kamanda Kenyela.
Akisimulia tukio hilo, Kamanda Kenyela, alisema Papaa Msofe
alikamatwa baada ya kutokea mauaji ya Onesphori Kituli, mkazi wa
Magomeni Mapipa, jijini Dar es Salaam.
Alisema kabla ya kutokea mauaji hayo, Papaa Msofe na marehemu
walikuwa wakigombea nyumba ambayo ilikuwa imewekwa rehani kwa Sh.
milioni 30.
Habari zaidi kuhusiana na tukio hilo ambazo hata hivyo
hazikuthibitishwa na Kamanda Kenyela, zinasema kuwa bado kuna mtu
mwingine ambaye anahusishwa na tuhuma hizo za mauaji, lakini mpaka sasa
hajakamatwa.
Kamanda Kenyela alifafanua kwamba Papaa Msofe alimpa marehemu
fedha hizo kwa makubaliano kwamba ikiwa atashindwa kuzilipa atachukua
nyumba yake.
Kabla ya mauji hayo ilidaiwa kwamba, Papaa Msofe na mwenzake walikuwa wakimtishia maisha marehemu huyo.
Kamanda Kenyela alisema kutokana na kuwepo kwa mgogoro huo,
marehemu alifungua kesi mahakamani na kwamba siku ya hukumu alikutwa
amekufa mbele ya mlango wa nyumba yake na kwamba hakuna mali yoyote
iliyochukuliwa.
Kwa mujibu wa Kamanda Kenyela, mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment