Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, August 27, 2012

SIMBA YACHINJA ARUSHA, AKUFFO AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO MSIMBAZI



Akuffo akishangilia baada ya kufunga



















































BAO la penalti dakika ya 81 lililofungwa na kiungo Kiggi Makassy, jioni hii limeipa Simba ushindi wa mabao 2-1  
dhidi ya Mathare United ya Kenya katika mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii kwenye 
Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.
Hadi mapumziko hakuna timu iliyofanikiwa kupata bao na kipindi cha pili, Simba SC inayofundishwa na Mserbia, 
Milovan Cirkovick ilipata bao la kuongoza dakika ya 53, mfungaji mshambuliaji kutoka Ghana, Daniel Akuffo 
aliyeunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu uliopigwa na Amir Maftah.   
Mathare walisawazisha bao hilo dakika ya 68, mfungaji Daniel Mwaura aliyeipasua ngome ya Simba SC, iliyokuwa 
ikiogozwa na Paschal Ochieng na Juma Nyosso.
Beki wa Mathare alimuangusha kwenye eneo la hatari, Uhuru Suleiman dakika ya 80 na ushei na refa akaamuru
 ipigwe penalti, iliyopachikwa kimiani kiufundi kwa guu la kushoto la Kiggi Makassy.
Simba ilicheza vizuri mechi hiyo, leo hii Haruna Moshi ‘Boban’ akirudishwa katika nafasi ya kiungo baada ya 
kupatikana kwa washambuliaji halisi. Alicheza kwa utulivu, akigawa vizuri mipira na hata kuwapokonya mipira 
viungo wa timu pinzani.
Dakika za mwishoni ilishuhudiwa Boban akipitia mpira kwa nguvu miguuni mwa mshambuliaji wa Mathare, baada
 ya Maftah kupitwa, kuashiria kwamba kijana amebadilika si Yule wa kukaba kwa macho.
Feliz Sunzu na Akuffo walikuwa wanapishana vizuri pale mbele na waliitia misukosuko ngome ya Mathare- zaidi ni
 kwamba wawili hawa wanahitaji muda zaidi wa kucheza pamoja ili kutengeneza safu kali ya ushambuliaji ya Simba SC.
Juma Kaseja na Mrisho Ngassa hawakushiriki kabisa mechi ya leo kwa sababu walikuwa wagonjwa na Keita 
alimpisha Nyosso baada ya kuumia.  
Simba itamenyana na Azam katika mechi ya Ngao ya Jamii ya kuashiria kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu ya 
Vodacom Tanzania Bara, Septemba 8, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kihistoria hiyo itakuwa mechi ya tano ya Ngao ya Jamii kuchezwa nchini na ya pili kuishirikisha timu nje ya 
wapinzani wa jadi wa soka ya Tanzania, Simba na Yanga.
Mtibwa ilicheza na Yanga mwaka 2009, baada ya Simba kugoma na ikashinda mabao 2-1 na kutwaa Ngao, 
wakati kabla ya hapo, mwaka 2001, Ligi Kuu ya Tanzania ikiwa bado inadhaminiwa na Kampuni ya Bia
 Tanzania (TBL), kupitia bia ya Safari Lager, ilichezwa mechi ya kwanza ya Ngao kihistoria.
Katika mechi hiyo, Yanga ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Simba na mwaka juzi Yanga iliifunga tena Simba kwa
 penali 3-1 kufuatia sare ya 0-0 na mwaka jana, Simba ilitwaa Ngao ya kwanza katika historia yake, kwa kuifunga
 Yanga mabao 2-0. 
Katika mchezo huo, kikosi cha Simba kilikuwa; Wilbert Mweta/Hassan Waziri, Nassor Masoud ‘Chollo’, Amir
 Maftah/Paul Ngalema, Paschal Ochieng, Komabil Keita/Juma Nyosso, Salum Kinje/Ramadhan Chombo ‘Redondo’,
 Mwinyi Kazimoto/Haruna Shamte, Haruna Moshi, Felix Sunzu, Abdallah Juma/Amri Kiemba na Daniel 
Akuffo/Uhuru Suleiman.


Keita akiwa benchi baada ya kuumia

Mabosi wapya wa Friends Of Simba, Zacharia Hans Poppe kushoto na
Adam Mgoyi kulia wakifuatilia mechi

Akuffo kulia

Akuffo kulia

Akuffo kulia

Beki Ochieng akiisaidia mashambulizi


Akuffo anapiga kichwa kufunga mbele ya mabeki wa mathare, pembeni yake  ni Ochieng na kulia kabisa ni Sunzu


Kipa Hamadi Waziri akimpongeza Akuffo baada ya kufunga


Sunzu

Akuffo anakosa bao la wazi

Akuffo anakosa bao

Akuffo anakosa bao.
source bin zubeiry

No comments:

Post a Comment