Kenya
imepokonywa fursa ya kuandaa mashindano ya mwaka huu ya kuwania kombe
la klabu bingwa kanda ya Afrika Mashariki na Kati Cecafa, kutokana na
maandalizi mabaya.
Kwa
mujibu wa katibu mkuu wa CECAFA, Nicolasa Musonye, shirikisho la mchezo
wa soka nchini Kenya, limeshindwa kuandaa mashindano hayo uamuzi ambao
umelazimisha mdhamini mkuu wa mashindano hayo kuipa fursa hiyo
shirikisho la mchezo wa soka nchini Uganda, kuyaandaa.
Shirikisho
la mchezo wa soka nchini Uganda FUFA, tayari limeteuwa jopo la watu
Kumi kuandaa mashindano hayo yatakayo andaliwa katika uwanja wa Namboole
mjini Kampala, kati ya tarehe 27 Novemba hadi tarehe 12 Decemba mwaka
huu.
Lakini Kenya na Sudan, ambayo inashiriki katika michuano hiyo kwa mara ya kwanza zimepinga uamuzi huo wa CECAFA.
Rais
wa shirikisho la mchezo wa soka nchini Sudan Kusini, Ghabur Goc Alei,
amesema atashinikiza nchi wanachama wa CECAFA, kuhakikisha uamuzi
uliochukuliwa na kamati kuu ya CECAFA kuhusu mwenyeji wa mashindano hayo
unatekelezwa.
Kenya
iliteuliwa kuandaa mashindano hayo na kamati kuu ya CECAFA wakati wa
mkutano wake ulioandaliwa mjini Dar es Salaam Decemba mwaka uliopita,
lakini katibu mkuu wa CECAFA anasema uamuzi huo umechukuliwa baada ya
wadhamini wa mashindano hayo kutaka iandaliwa mjini Kampala
No comments:
Post a Comment