UNATAKA
KUMJUA ANAYEKUIBIA MUMEO?. MBINU HIZI ZITAKUFAA!. |
Ikague
simu yake
Katika
mazingira ya kawaida, haishauriwi kuikaguakagua simu ya mumeo kwani kufanya
hivyo ni kuonesha jinsi usivyomuamini lakini unapohisi unaibiwa na hujui ni
nani mwizi wako, unaweza kuanza kuikagua simu ya mpenzi wako kwa siri sana.
Angalia simu zilizoingia na kutoka, meseji zilizotumwa na kuingia. Kama kuna
mtu ambaye ana uhusiano naye, utagundua lakini tambua kwamba ni zoezi la muda
mrefu na fanya hivyo bila mpenzi wako kugundua. Tumia muda anaokwenda kuoga,
chooni na anapoisahau simu nyumbani, ipo siku utabaini siri nzito.
.
Ingia
kwenye Facebook yake
Kama mumeo
ni mtu wa facebook na unajua password yake, ingia mara kwa mara kwenye ukurasa
wake. Kama ulikuwa hujui mtandao huo wa kijamii sasa hivi unatumiwa na wengi
katika kuzisaliti ndoa zao. Waume za watu wanatumia njia hiyo kuwasiliana na
vimada baada ya kubaini wakitumia simu ni rahisi kukamatwa. Kwa maana hiyo,
tumia mbinu ya ushawishi kupata password yake na huko unaweza kumbaini mtu
anayekuharibia.
3. Mfanyie
sapraizikazini
Kama mumeo
anafanya kazi, elewa kwamba wengi hutumia muda wa kuwa na wapenzi wao wa pembeni. Unaweza
kumuibukia siku mojamoja kazini kwake au kwenda sehemu ambayo hupendelea kula
chakula cha mchana.
Kwa mfano
siku ya kwanza umemkuta yuko na demu, ukaondoka kisha siku nyingine ukawakuta
tena pamoja, ukaondoka na siku nyingine tena ukawaona katika mazingira hayo,
akili yako itakupa jibu. Hata hivyo, katika njia hii uwe makini kwani
inawezekana huyo msichana ni mfanyakazi mwenzake ambaye hupendelea kwenda naye
lunch tu na hakuna kingine cha zaidi
4.
Chunguza nguo zake unapozifua
Wakati
unafua nguo zake, tumia muda mwingi kuzichunguza. Angalia kwenye waleti yake,
unaweza kukutana na risiti zinazoonesha amenunua vitu vya kike ambavyo wewe
hujaviona. Pia unaweza kukutana na vikaratasi vyenye namba za simu ambazo
ukizipiga ni za mwanamke na ukimwambia wewe ni mke wa fulani, anakupa majibu ya
kiwiziwizi. Pia kwenye nguo zake unaweza kubaini nyekundu wakati wewe hutumii hiyo.
5. Muazime
gari lake
Kama
mpenzi wako analo gari, mshitukize kisha muombe gari lake uende sehemu. Kwa
kumshitukiza atakuwa hajapata nafasi ya kulisafisha hivyo ukiwa nalo lichunguze
kila sehemu. Unaweza kukutana na risiti, namba za simu au nguo na vitu vya kike
ambavyo huvijui. Wapo ambao waliwahi kufanya hivyo na wamefanikiwa kubaini
usaliti wanaofanyiwa.
6.
Mshitukize baa
Yawezekana
mumeo ni mnywaji wa pombe na umekuwa ukimpa uhuru wa kufanya hivyo bila
kumfuatilia. Kama umebaini unasalitiwa na humjui anayekuibia penzi lako, siku
moja muulize anakunywa pombe wapi, kwa kuwa amezoea huna tabia ya kumfuatilia,
atakujibu. Siku hiyo mfuate, mwanamke utakayemkuta naye mnoti kisha ondoka bila
mpenzi wako kujua. Siku nyingine, mbabatize tena akiwa baa na kama utamkuta na
msichana yuleyule, basi mwekee alama na kwa uchunguzi ambao utaendelea nao,
kuna siku utajua ukweli.
7.
Mfuatilie
Hili
nalo halishauriwi kulifanya kwani mpenzi wako akijua unamfuatilia, anaweza
kukuacha kwani atajua humuamini na wengi hawapendi kuendelea kuishi na watu
ambao hawawaamini. Ila sasa, ukishahisi unasalitiwa huna budi kufanya hivyo.
Tumia watu kufuatilia nyendo zake kila anapokwenda na haitachukua siku nyingi
utajua huyo mpenzi wako anakusaliti na mtu gani.
Kwa kifupi
ni kwamba, unastahili kuwa na mtu muaminifu, anayekujali na kukupenda kwa
dhati. Unapohisi mumeo si muaminifu, usikimbilie kuomba talaka au kuja juu kama
moto wa kifuu bila kuwa na ushahidi. Tumia mbinu hizo hapo juu kutafuta
ushahidi wa kile unachokihisi na mwishowe utafanya uamuzi sahihi
No comments:
Post a Comment